Alichokiongea Jaji Kiongozi na Wataalamu kutoka Benki ya Dunia, hiki hapa


Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dkt, Eliezer Feleshi, amefanya mazungumzo na wadau kutoka Benki ya Dunia(WB) juu ya tathmini ya  Mradi wa Maboresho ya Mahakama ya Tanzania  yanayofanywa chini, ambapo umeleta matokeo chanya katika shughuli za Mahakama.

 Akizungumza  na ujumbe wa benki hiyo, katika ofisi za  Mahakama Kuu ya Tanzania, Jaji Kiongozi  alisema  mradi huo, umeweza kusaidia kuboresha shughuli za utendaji kazi wa Mahakama na kusogeza huduma karibu na wananchi.

“Tumeweza kusikiliza kesi kwa kutumia Mahakama Inayotembea (Mobile Court) jijini Mwanza, hivyo ni moja ya maboresho ya huduma za Mahakama, yaliyotokana na mradi huu,” alisema  Jaji Kiongozi.

 Aliongeza kuwa mradi huo unaofadhiliwa kwa fedha za mkopo kutoka benki hiyo,  umewezesha  Mahakama ya Tanzania,kusikiliza kesi kwa njia ya Mtandao ‘Video coference’, ambapo, ugeni huo, ulitaka kufahamu tathimini ya eneo hilo, alisema  umeweza kutumika   katika baadhi ya mikoa,ambayo ni  Mbeya, Bukoba, na Kituo cha Mafunzo cha kilichopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyo-Dar es Saalam, kikiwemo Chuo cha  Uongozi wa Mahakama(IJA) Lushoto.

Jaji  Kiongozi amefafanua  mkakati wa kupata ukumbi(chumba maalum) kwa ajili ya  kuanzisha kusikiliza kesi  kwa njia ya mtandao  katika gereza la Keko Jijini Dar es Salaam.

Jaji kiongozi amefafanua changamoto zinazoikabili Mahakama ikiwa ni pamoja na  upungufu wa kumbi maalumu za kuendeshea kesi kwa njia hiyo,‘Tunakabiliwa na upungufu wa kumbi maalumu kwa ajili ya kuendeshea kesi, hivyo tunatakiwa tupate kumbi nyingi ili tuweze kuendesha kesi kwa wakati.

 Aliongeza kwamba kwa hivi sasa ni ukumbi mmoja ndio unaotumika kuendesha kesi kwa njia hiyo, " alisema, Dkt. Jaji Kiongozi.

Aliyataja mafaniko mengine  ni  Mfumo wa Kusajili kesi kwa njia ya   Kielektroniki(JSDS).

Dkt. Feleshi  alisema eneo lingine, ambalo litafanyikazi ni kuhusu ambayo  upelelezi wa kesi  kuchukua muda mrefu ambapo kesi moja inaweza kuchukua kati ya mwaka mmoja au zaidi, hivyo litawekewa muda maalum.




Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato