Dkt. Kigwangalla azindua kampeni ya 'Twenzetu Kutalii'
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizindua rasmi Kampeni ya “Twenzetu Kutalii” iliyoandaliwa na MISS Tanzania 2018, Queen Elizabeth Makune kuhamasisha Utalii wa ndani katika hoteli ya Serena, Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo, Dkt. Kigwangalla amewapongeza waandaaji wa tukio hilo kwa kuunga mkono juhudi za Serikali za kutangaza Utalii ndani na nje ya nchi.
Amesema ipo haja ya viongozi na watu mashuhuri wakiwemo Wasanii kutumika kutangaza Utalii nchini. Amewataka wasanii wa Filamu waandae Filamu itakayoonesha na kubeba maudhui ya kuvitangaza Vivutio vya Utalii vilivyopo hapa nchini.
Aidha, ameiagiza Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) iendelee kutoa ushirikiano kwa Balozi huyo wa Utalii MISS Tanzania 2018/2019, Queen Elizabeth Makune kutokana na juhudi zake za kutangaza Utalii kwa vitendo.Pia ameiagiza TANAPA ianze kufanya mchakato wa kununua Meli mpya ya Kitalii itakayotumika Pwani ya Bahari ya Hindi.
Comments
Post a Comment