Makamu Mwenyekiti mpya apatikana Halmashauri ya Hai


Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro, limefanya uchaguzi na kumchagua, Elingaya Massawe kuwa Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Baraza hilo limefanya uchaguzi huo Ijumaa hii, chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wake Helga Mchomvu.

Massawe aliibuka mshindi baada ya kupata kura 15 kati ya 22 zilizopigwa na kumshinda mshindani wake Deo Kimaro ambaye alipata kura saba.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato