Posts

Showing posts from December, 2018

VIDEO: Rais Magufuli atuma salamu za Mwaka Mpya kwa aina yake

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri ya Mwaka Mpya wa 2019 Watanzania wote na kuwaomba wadumishe umoja, amani na upendo waliouonyesha katika mwaka 2018. TAZAMA FULL VIDEO HAPA, PIA SUBSCRIBE 

Matukio katika picha; Show ya Alikiba na Sauti Sol Mombasa

Image
Usiku wa kuamkia leo msanii wa Bongo Fleva, Alikiba alikuwa na show Mombasa nchini Kenya. Katika show hiyo iliyoandaliwa na NRG Radio, Alikiba alitumbuiza na kundi la muziki kutoka nchini humo, Sauti Sol ambayo wamewahi kufanya wimbo mmoja pamoja.

Mkurugenzi wa Dodoma atoa ripoti ya utendji kazi

Image
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi ametoa ripoti ya utendaji kazi uliofanywa na Ofisi yake katika kipindi cha mwaka 2018, Mkurugenzi huyo ametoa ripoti hiyo wakati akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake na kusema kuwa mpango wao ifikapo mwaka 2020 na 2021 wajitegemee kwa asilimia 100 kama Majiji mengine duniani kupitia mapato ya ndani. Pia amesema sasa hivi wameanza kulipa Maji, Umeme na Walinzi katika Shule Jijini humo, Mwaka ujao amesema wataanza kuwalipa posho zote za Watumishi Serikali kuu ibaki na mishahara tuu. " Kwamujibu wa mpango wetu ifikapo 2020 na 2021 tujitegemee kwa asilimia 100 kama Majiji mengine duniani sisi tunataka tufikie huko, Mwaka ujao tutaanza kuwalipa posho zote za Watumishi Serikali kuu ibaki na mishahara tu" alisema Kunambi

Jibu la Gigy Money kuhusu kurudiana na MO J

Image
Msanii wa muziki Bongo na Video Vixen, Gigy Money amejibu iwapo amerudia na mpenzi wake Mo J baada ya hivi karibuni kuonekana pamoja na mtoto wao. Mwanadada huyo maarufu mtandaoni akizungumza na Wasafi TV amesema ni kweli kwa sasa wapo pamoja na hawajawahi kuachana. "Unajua kuachana ni maneno tu tunakuwa tunaongea, halafu tukiachana sisi kwa ajili tayari ni wazazi kimaadili yetu tutakuja kukutanishwa tu na yule mtoto pale ndani, angalieni tu vitendo (tumerudiana)," amesema Gigy Money. Utakumbuka baada ya Gigy Money kujifungua kuliibuka mvutano kati yake na Mo J ambaye ni Mtangazaji wa Choice FM kwa madai kuwa mtoto si wake baadaye zikaibuka tuhuma nyingine kuwa hatoi matunzo kwa mtoto lakini sasa wameonekana pamoja na wenye furaha.

Wakamatwa na vifurushi 23 vya bangi na Marobota

Image
Watuhumiwa watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita kwa tuhuma za kupatikana na marobota ya bangi mawili na vifurushi 23, mamlaka ya mji mdogo wa Katoro, wilayani Geita. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwaburambo, akithibitisha kuwapo kwa tukio hilo jana aliwataja watuhumiwa hao kuwa Emmanuel Magige (24), Imani Daudi (18) na Sirilo Jephta (18), ambao wote wanashikiliwa kwa kuhusishwa na tukio hilo. Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo, Kamanda Mponjoli, alisema uzito na thamani ya bangi iliyokamatwa vilikuwa bado vinafanyiwa kazi, hata hivyo, uchunguzi wa awali umebainisha kuwa bangi hiyo ilikuwa imeingizwa mkoani Geita kutoka wilayani Uyuyi, mkoani Tabora. ''Hili ni tukio la kwanza la kukamatwa bangi kwa wingi kiasi hiki toka Mkoa wa Geita kuanzishwa rasmi mwaka 2012,'' alisema Kamanda Mwaburambo. Alisema bangi hiyo ilikuwa inatarajiwa kusambazwa katika maeneo yenye shughuli za uvuvi na machimbo ya madini ikiwamo katika visiwa vilivyopo katik...

Rais Magufuli atoa angalizo Mwaka Mpya, 'Kila wanalolifanya wanasema ni maagizo kutoka juu'

Image
Rais John Pombe Magufuli amewatakia heri ya Mwaka Mpya wa 2019 Watanzania wote na kuwaomba wadumishe umoja, amani na upendo waliouonesha katika mwaka 2018. Akizungumza kutoka nyumbani kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam,  Rais Magufuli amesema mwaka 2018 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa Watanzania na anatarajia kuwa mwaka 2019 utakuwa wa mafanikio zaidi kulingana na mipango ambayo nchi imejipangia kuitekeleza. Rais Magufuli amewataka watumishi wa umma, viongozi, wakulima, wafanyabiashara, wavuvi na wafugaji kuongeza juhudi za uzalishaji mali katika mwaka 2019 huku wakipiga vita rushwa, wizi, ufisadi, ubadhilifu na kwamba anaamini kuwa uchumi wa Tanzania utazidi kupanda katika mwaka 2019. “Ujumbe wangu kwa watumishi wa umma, ni kama nilivyotoa ujumbe kwa Watanzania wengine, wachape kazi, wajiamini, waachane na utamaduni wa kila kitu wanachokifanya kudai ni maagizo kutoka juu, huo ni ugonjwa ambao umeanza kuwapata watumishi wa umma ambapo kila wanalolifanya hata kama ni kwa mujib...

Nikki wa Pili atoa namna ya kuishi vizuri mwaka 2019

Image
Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Nikki wa Pili ameeleza mambo kadhaa ya kuzingatia ili mwaka 2019 uwe wenye mafanikio na furaha kwako kwa ujuma. Rapa huyo kutoka kundi la Weusi ameeleza kujali afya ndio kitu cha kwanza kabisa, pia kufanya vitu ambavyo wanaokuzunguka hawakutegemea hilo. "Mwaka 2019 fanya kile ambacho hakuna aliyetegemea utafanya, kuwa kile ambacho wanaamini huwezi kuwa.usijaribu tena kuuishi mwaka 2018 umeshapita acha na mambo yake yapite, kama vile mwaka mpya umekuja bila kujiuliza na wewe usiogope mabaliko," ameandika Nikki kwenye ukurasa wake wa Twitter na kuendelea.  "Jijali tumia kinga, kunywa kwa kiasi, fanya mazoezi, punguza marafiki mzigo, timiza majukumu kuwa positive, mpende sana mpenzi wako, mitando ina chochea stress (msongo wa mawazo) kama utajali kila ukionacho au ukisomacho, sema ukweli mara nyingi, jiandae kudhibiti mapungufu yako kuwa mfano bora," ameeleza Nikki wa Pili. Licha ya kufanya muziki wa hip hop kwa kipindi kire...

Adakwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua Mama yake mzazi kwa Kisu

Image
Mkazi wa Kijiji cha Moleti Wilaya ya Kongwa Peter Mgomba (26), anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kumuua mama yake mzazi kwa kumchoma kisu tumboni. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, alisema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari, jiijini hapo jana. Kamanda Muroto alisema tukio hilo lilitokea Desemba 29, katika Kijiji cha Moleti, Tarafa Mlali, Wilaya ya Kongwa. Alisema tukio la mauaji linadaiwa kufanyika wakati Mgomba alipomchoma kisu tumboni mama yake mzazi, Anita Mgomba (61) na kusababisha kifo. Alisema chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika, lakini wanaendelea na uchunguzi na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani. Hata hivyo, Kamanda Muroto alisema mtuhumiwa anasadikiwa kuwa ni mgonjwa wa tatizo la akili na baada ya kufanya tukio alitoroka, lakini jeshi hilo lilimtafuta na kumtia nguvuni. Alisema siku ya tukio, Anita alijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini, lakini akiwa kwenye matibabu Desemba 30, alifariki dunia. Wakati huo huo, K...

Tanzania Prisons watafuta njia kurudi kwenye ubora

Image
Kikosi cha Tanzania Prisons msimu uliopita walimaliza wakiwa nafasi ya nne huku Kocha wao Mkuu, Mohamed Abdallah akipewa tuzo ya Kocha Bora wa msimu uliopita. Kikosi hicho msimu huu kinawaumiza mashabiki na Viongozi kutokana na kushindwa kufurukuta kwa michezo ambayo wamecheza Ligi Kuu. Kwa sasa Prisons wamecheza michezo 18 wameshinda mchezo mmoja pekee na kutoa sare michezo 9, wamepoteza michezo 8 na kujikusanyia pointi 12 wakiwa nafasi ya 19 kwenye msimamo wa Ligi hali iliyofanya wamtimue kazi kocha wao.  Beki wa kikosi hicho Salum Kimenya amesema kuwa wanatambua kazi kubwa waliyonayo katika kupata matokeo hivyo wataongeza juhudi kuweza kujinasua katika nafasi waliyopo kwa sasa. "Hatupo sehemu nzuri, tuna kazi kubwa kutoka hapa tulipo na njia ni moja tu kupata matokeo mazuri katika michezo yetu mashabiki watupe sapoti," alisema.

MAGAZETI YA LEO 1/12/2019

Image

Sababu kuu 7 za kwanini kila mwanaume anahitaji mwanamke sahihi

Image
Kwangu kipindi ambacho kilinivutia sana ni kipindi cha kampeni za uchaguzi nchini Marekani. Ni pale Obama akiwa katika kampeni kwenye moja ya majimbo kugombea duru ya pili ya uraisi aliposimamisha hotuba yake na kutambua uwepo wa mkewe Michelle. Obama alisema, "Mke wangu amekuwa bega kwa bega na mimi tokea niko chuo, kuna kipindi nilishindwa kulipa ada ila yeye ndiye aliyenilipia" Obama akaenda mbali zaidi na kukiri mbele ya jamii ya kimataifa kwamba asingekuwepo hapo alipo kama sio mke wake Michelle. Hivyo basi, nashauri kwamba mwanamke ambae mwanaume atakua nae huenda akawa chachu ya mafanikio na baraka kwake au anaweza akamrudisha nyuma kabisa katika mipango yake. Sababu kuu 7 za kwanini iwe isiwe mwanaume lazima upate mwanamke alie sahihi. 1. Kila mwanamke anao uwezo wa kukuridhisha kimapenzi ila mwanamke sahihi na bora pekee ndiue anaeweza kuku-challenge kiakili na kuwa 'intellectually inspired'. 2. Mwanamke yeyote anaweza kukuteka kihisia, ila y...

HAPPY NEW YEAR 2019

Image
Mkurugenzi na wafanyakazi wote wa Muungwana Blog tunawatakia wasomaji wetu wote wa Tovuti yetu na kurasa zetu za Facebook, Twitter na Instagram heri ya Mwaka Mpya 2019. Tunawatakia baraka na mafanikio mema kwa mwaka huu tuliouanza leo.

Mambo yatakayokusaidia uweze kuamka mapema kila siku

Image
Katika karne hii zipo  sababu mbalimbali zinazowafanya watu wachelewa kuamka. Hivyo kama na wewe ni miongoni mwa watu wanaochelewa kuamaka kila siku basi unatakiwa kufanya mambo yafutayo: 1. Iwekee Kipaumbele kazi unayopenda kufanya  zaidi iwe ya kwanza kutendeka asubuhi. Utajikuta unatamani kuamka mapema zaidi kuwahi kazi hiyo na siku yako itaenda vizuri. 2. Kuna chakula/tunda unalolipenda zaidi? Jiwekee zawadi, kwamba ukiamka asubuhi tu cha kwanza ni kula chakula hicho/ tunda/ chokleti nk. Hii itakufanya Utoke kitandani pale tu atakaposhtuka.                                                                                                  3. Andaa mapema nguo ya kuvaa siku inayofuatia, ili kuwahi jumatatu, andaa nguo ya kuvaa ju...

Faida ya kunywa chai ya tangawizi kiafya

Image
Ili uweze kuwa na afya bora kila wakati unashauriwa kutumia chai ya tangawizi kwa wingi ili uweze kujikinga na kutibu magonjwa mbalimbali.  Zifutazo ndizo faida ya kunywa chai ya tangawizi. Huondoa Harufu mbaya ya kinywa. Tofauti na vyakula vingine kama kitunguu swaumu, tangawizi husaidia uwe na harufu nzuri pale unapopumua na kufanya maeneo ya kinywa chako  kuwa safi. Tangawizi husaidia msukumo wa damu Tangawizi husaidia msukumo wa damu mwilini kwasababu huupa mwili joto ambalo mara nyingi mwili huhitaji wakati wa usukumwaji wa damu mwilini. Huondoa Magonjwa ya asubuhi Licha ya kuwa tiba ya magonjwa kama Kikohozi na Mafua, Tangawizi pia husaidia kupunguza magonjwa ya asubuhi kama uchovu, na mning’inio. Kwa akina mama wajawazito, Tangawizi huwapunguzia homa za asubuhi pindi wanapoamka, pia hutumika kama kichocheo cha utulivu. Tangawizi husaidia mfumo wa chakula Husaidia mwili kunyonya virutubisho kwenye chakula. Hii husaidiana sana pale unapoamua kupunguza uzito w...

Namna sahihi ya kuongeza uwezo wako wa kumbukumbu

Image
Jifunze kufanya kazi moja kwa wakati mmoja. Kama unajifunza kitu basi jifunze kitu kimoja kwa wakati/siku moja. Hii itaepusha kuchanganya mambo utakapokuwa unakumbuka Tafuna  Bazoka (chewing gum) unapofanya kazi inayohitaji kumbukumbu kubwa au unaposoma kitu kipya. Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya saikolojia, utafunaji wa bazoka hufanya misuli ya kichwa kuwa “active” . Fanya mazoezi ya viungo kama kukimbia, pushup, kuendesha baiskeli nk! Kunja ngumi  unapojifunza au kukumbuka jambo! Hii inaweza kukuchekesha na ikawa rahisi sana lakini utafiti unaonesha kuwa, watu wanaokunja mmoja wa mikono yao wanapojifunza/kusoma, huwa na kumbukumbu zaidi ya wasiokunja ngumi. Punguza kiasi cha kunywa pombe kwani unywaji wa pombe kupita kwaida, huathiri pia seli za kichwa na kuathiri uwezo wako  wa kukumbuka mambo na kuwa makini. Cheza game za kutumia akili kama “draft”, puzzle, na mengineyo. Lala masaa ya kutosha. Binadamu anatakiwa kulala masaa 7 mpaka 9 kila siku. Kulal...

Njia sahihi ya kuikuza biashara yako

Image
Kwa Kuwa kuna usemi  wanasema wengi wape na kwaku kuwa takwimu sinatuambia  idadi kubwa ya watu ni wafanyabiashara ni vyema tukakumbiashara baadhi ya mambo ya msingi yatakayotufanya ili kukuaza biashara zetu . Na asilimia 40 ya watu ambayo hawafanyi  biashara ni muda wao na wenyewe kujifunza ili waweze nao kuwa wafanyabiashara wazuri. Moja ya changamoto kubwa inayokuwakumba wafanyabiashara walio wengi ni kutokujua kiundani juu ya biashara yake hata hivyo idadi kubwa ya wafanyabiashara hao biashara zao huwa haziwi za muda mrefu na hata pale zinapokuwa za muda mrefu huwa hazikui. Nakusihi ufuatane nami mwanzo hadi mwisho ili kuweza kuona biashara yako inakuwa na Maisha marefu na yenye kukua. 1.  Ongeza maarifa kwa kujifunza. Kama kweli unahitaji Mafanikio zaidi ya kiabiashara ni vyema ukawa ni mtu wa kujifunza kuhusiana na biashara yako. Ni lazima ujifunze mbinu mbalimbali ambazo wanazitumia wafanyabiashara wengine. Kujifunza huku kujupe muda muafaka wakugundua p...

Dkt. Shein atoa risala ya kuukaribisha mwaka mpya

Image
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi  wa Zanzibar kuendelea kuidumisha hali ya amani na utulivu. Dk. Shein aliyasema hayo leo katika risala yake ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2019 aliyoitoa kupitia vyombo vya habari, Ikulu mjini Zanzibar. Katika risala yake hiyo Rais Dk. Shein alieleza kuwa hali ya amani, umoja na mshikamano uliopo nchini ni jambo muhimu linalowavutia Washirika wa maendeleo ambao wanaridhika na jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ndio maana wanaiunga mkono katika mipango yake ya maendeleo. Hata hivyo, Dk. Shein alitoa shukurani nyingi kwa wananchi wote kwa kuunga mkono juhudi za Serikali za kuiletea maendeleo Zanzibar ambapo moyo wao huo wa umoja na mshikamano umewezesha kuimarisha vizuri hali ya uchumi wa Zanzibar. Aidha, Rais Dk. Shein alisisitiza kuwa wakati unakaribishwa mwaka 2019 ni wajibu wa kila Taasisi ya Serikali ikajipima namna inavyoendelea kutekeleza mambo yaliyoagizwa katika Ilani ya CCM ya...

Samir Nasri arejea ligi kuu ya Uingereza

Image
Mchezaji Samir Nasri amejiunga na klabu ya West Ham ambapo ataitumikia klabu hiyo hadi mwisho wa msimu huu. Nasri alishawahi kuchezea vilabu vya Arsenal na Man City kwa nyakati tofauti katika ligi kuu ya Uingereza.

Jumla vyumba 250 vya madarasa vyahitajika Tabora

Image
Mkuu wa Mkoa Tabora, Aggrey Mwanri amesema jumla vyumba 250 vya madarasa vinahitajika kwa ajili ya wanafunzi 12,402 waliofaulu mtihani wa darasa la saba lakini hawakuchaguliwa kwa sababu ya uhaba wa madarasa. Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa huyo alipokuwa akizungumza na watumishi wa Mkoa na kutoa salamu kwa wananchi za kuuaga mwaka 2018 na kuukaribisha mwaka 2019. Alizitaka Halmashauri zote kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha wanajenga haraka vyumba vya madarasa kwa ajili ya kuhakikisha wanafunzi hao waliofauli lakini wamekosa nafasi kwa sababu ya uhaba wa vyumba wanaanza masomo. Mwanri alisema azma ya Mkoa wa Tabora ni kuhakikisha kila mtoto anayefaulu aendelee na masomo hadi afike Chuo Kikuu na sio kuishia njiani kwa sababu ya kukosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza kwa sababu ya ukosefu wa madarasa. Jumla ya wanafunzi 17,414 wakiwemo wavulana 8,120 na wasichana 9,294 sawa na asilimia 60 ya wanafunzi  wote waliofaulu mtihani waliochaguliwa k...

Chelsea yakataa ofa ya Bayern Munich

Image
Klabu ya Chelsea imekataa dau la zaidi ya paundi milioni 20 kutoka kwa klabu ya Bayern Munich kwaajili ya mchezaji Callum Hudson-Odoi, Sky Sports News understands. Chelsea imeiambia Bayern kwamba nyota wao huyo anathamani ya paundi milion 40. Wapinzani wa Bayern kalika ligi kuu ya Ujerumani Borussia Dortmund nayo inamuhitaji mchezaji huyo ambaye mkataba wake na klabu ya Chelsea unamalizika mwaka 2020.

Mayweather ampiga 'knockout' mara tatu Tenshin Nasukawa

Image
 Floyd Mayweather alihitaji sekunde 140 pekee kumshinda mpinzani wake wa Japan Tenshin Nasukawa katika pigano la maonyesho lililokuwa na thamani ya dola $9m. Bingwa huyo mara tano wa zamani Mayweather mwenye umri wa miaka 41 alikuwa akitabasamu wakati wa pigano hilo la muda mfupi mjini Tokyo alipombwaga mara tatu mpinzani wake mwenye umri wa miaka 20. Pigano hilo la raundi tatu lilimalizika huku Nasukawa akibubujikwa na machozi baada ya kikosi chake kurusha kitambaa cheupe ndani ya ulingo kikitaka pigano kusitishwa. Licha ya kurudi katika pigano hilo Mayweather alisema yeye amestaafu ndondi za kulipwa. ''Ni hatua ya kuburudisha tu, tulifurahia sana , alisema raia huyo wa Marekani ambaye alimshinda bingwa wa UFC Conor McGregor katika pigano la masumbwi mnamo mwezi Agosti 2017. ''Walitaka pigano hili kufanyika nchini Japan hivyobasi nikasema kwa nini lisifanyike?'' Pigano hilo lilicheleweshwa kwa saa kadhaa huku kukiwa na uvumi katika mitandao ya ki...

Mfumo Bora wa udhibiti chakula, TFDA yaongoza Afrika

Image
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA),  imetambulika kufikia ngazi ya tatu (Maturity Level 3) ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya ubora wa mfumo wa udhibiti wa dawa, hatua ambayo imeifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kupata mafanikio hayo. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, kuhusu mafanikio ya taasisi hiyo katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Adam Fimbo, alisema kuwa TFDA imepata mafanikio hayo makubwa  kutokana na kuwa na mifumo thabiti ya udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa dawa, ambapo Desemba mwaka huu, imetambulika kufikia ngazi ya tatu (Maturity Level 3) ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya ubora wa mfumo wa udhibiti wa dawa, hatua ambayo imesaidia  Tanzania kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufikia  hatua hiyo muhimu. “Hii ni hatua kubwa kwa kuwa taasisi ya mfano barani Afrika katika udhibiti wa bidhaa za chaku...