Jumla vyumba 250 vya madarasa vyahitajika Tabora


Mkuu wa Mkoa Tabora, Aggrey Mwanri amesema jumla vyumba 250 vya madarasa vinahitajika kwa ajili ya wanafunzi 12,402 waliofaulu mtihani wa darasa la saba lakini hawakuchaguliwa kwa sababu ya uhaba wa madarasa.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa huyo alipokuwa akizungumza na watumishi wa Mkoa na kutoa salamu kwa wananchi za kuuaga mwaka 2018 na kuukaribisha mwaka 2019.

Alizitaka Halmashauri zote kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha wanajenga haraka vyumba vya madarasa kwa ajili ya kuhakikisha wanafunzi hao waliofauli lakini wamekosa nafasi kwa sababu ya uhaba wa vyumba wanaanza masomo.

Mwanri alisema azma ya Mkoa wa Tabora ni kuhakikisha kila mtoto anayefaulu aendelee na masomo hadi afike Chuo Kikuu na sio kuishia njiani kwa sababu ya kukosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza kwa sababu ya ukosefu wa madarasa.

Jumla ya wanafunzi 17,414 wakiwemo wavulana 8,120 na wasichana 9,294 sawa na asilimia 60 ya wanafunzi  wote waliofaulu mtihani waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza na walibaki 12.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato