Namna sahihi ya kuongeza uwezo wako wa kumbukumbu

Jifunze kufanya kazi moja kwa wakati mmoja. Kama unajifunza kitu basi jifunze kitu kimoja kwa wakati/siku moja. Hii itaepusha kuchanganya mambo utakapokuwa unakumbuka

Tafuna  Bazoka (chewing gum) unapofanya kazi inayohitaji kumbukumbu kubwa au unaposoma kitu kipya. Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya saikolojia, utafunaji wa bazoka hufanya misuli ya kichwa kuwa “active” .

Fanya mazoezi ya viungo kama kukimbia, pushup, kuendesha baiskeli nk!

Kunja ngumi  unapojifunza au kukumbuka jambo! Hii inaweza kukuchekesha na ikawa rahisi sana lakini utafiti unaonesha kuwa, watu wanaokunja mmoja wa mikono yao wanapojifunza/kusoma, huwa na kumbukumbu zaidi ya wasiokunja ngumi.

Punguza kiasi cha kunywa pombe kwani unywaji wa pombe kupita kwaida, huathiri pia seli za kichwa na kuathiri uwezo wako  wa kukumbuka mambo na kuwa makini.

Cheza game za kutumia akili kama “draft”, puzzle, na mengineyo.

Lala masaa ya kutosha. Binadamu anatakiwa kulala masaa 7 mpaka 9 kila siku. Kulala usingizi wa kutosha huufanya ubongo wako kupata muda wa kutosha wa kupumzika na kuongeza uwezo wako wa kukumbuka mambo.

Epuka kuwa na msongo wa mawazo kwani huharibu baadhi ya seli za ubongo na kuathiri uwezo wa kumbukumbu zako.

Kula chakula chenye madini ya chuma kwa wingi hasa matunda na mbogamboga.

Kujipa muda wa kukaa peke yako na kutafakari (Meditation). Kaa peke yako eneo lenye uoto wa asili kama bustanini, mtoni, au ufukweni na kujipa muda wa kutafakari. Hili ni moja ya mazoezi bora zaidi kwa ajili ya afya yako.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato