Wakamatwa na vifurushi 23 vya bangi na Marobota


Watuhumiwa watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita kwa tuhuma za kupatikana na marobota ya bangi mawili na vifurushi 23, mamlaka ya mji mdogo wa Katoro, wilayani Geita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwaburambo, akithibitisha kuwapo kwa tukio hilo jana aliwataja watuhumiwa hao kuwa Emmanuel Magige (24), Imani Daudi (18) na Sirilo Jephta (18), ambao wote wanashikiliwa kwa kuhusishwa na tukio hilo.

Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo, Kamanda Mponjoli, alisema uzito na thamani ya bangi iliyokamatwa vilikuwa bado vinafanyiwa kazi, hata hivyo, uchunguzi wa awali umebainisha kuwa bangi hiyo ilikuwa imeingizwa mkoani Geita kutoka wilayani Uyuyi, mkoani Tabora.

''Hili ni tukio la kwanza la kukamatwa bangi kwa wingi kiasi hiki toka Mkoa wa Geita kuanzishwa rasmi mwaka 2012,'' alisema Kamanda Mwaburambo.

Alisema bangi hiyo ilikuwa inatarajiwa kusambazwa katika maeneo yenye shughuli za uvuvi na machimbo ya madini ikiwamo katika visiwa vilivyopo katika Ziwa Victoria.

Alisema mchakato wa hatua za kuchukuliwa na uchunguzi kubaini thamani na uzito wa bangi iliyokamatwa unafanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mawakili wa serikali.

Akizungumzia kukamatwa kwa bangi hiyo, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ludete, Aloys Kamuli, alisema bangi hiyo ingefanikiwa kuifikia jamii anaamini ingeacha madhara makubwa.

Elias Mtoni, Mwenyekiti wa Mtaa wa Shilabela, Geita Mijini, akizungumzia kukamatwa kwa bangi hiyo, alisema madhara ya dawa za kulevya kwa vijana ni vita inayoihusisha jamii na siyo Jeshi la Polisi pekee.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato