Nikki wa Pili atoa namna ya kuishi vizuri mwaka 2019
Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Nikki wa Pili ameeleza mambo kadhaa ya kuzingatia ili mwaka 2019 uwe wenye mafanikio na furaha kwako kwa ujuma.
Rapa huyo kutoka kundi la Weusi ameeleza kujali afya ndio kitu cha kwanza kabisa, pia kufanya vitu ambavyo wanaokuzunguka hawakutegemea hilo.
"Mwaka 2019 fanya kile ambacho hakuna aliyetegemea utafanya, kuwa kile ambacho wanaamini huwezi kuwa.usijaribu tena kuuishi mwaka 2018 umeshapita acha na mambo yake yapite, kama vile mwaka mpya umekuja bila kujiuliza na wewe usiogope mabaliko," ameandika Nikki kwenye ukurasa wake wa Twitter na kuendelea.
"Jijali tumia kinga, kunywa kwa kiasi, fanya mazoezi, punguza marafiki mzigo, timiza majukumu kuwa positive, mpende sana mpenzi wako, mitando ina chochea stress (msongo wa mawazo) kama utajali kila ukionacho au ukisomacho, sema ukweli mara nyingi, jiandae kudhibiti mapungufu yako kuwa mfano bora," ameeleza Nikki wa Pili.
Licha ya kufanya muziki wa hip hop kwa kipindi kirefu, Nikki wa Pili ni msomi anayechukulia PhD kwa sasa na amekuwa akiitwa sehemu mbalimbali kuzungumza na vijana kwa kutoa mada kama puplic Speaker.
Comments
Post a Comment