Jibu la Gigy Money kuhusu kurudiana na MO J
Msanii wa muziki Bongo na Video Vixen, Gigy Money amejibu iwapo amerudia na mpenzi wake Mo J baada ya hivi karibuni kuonekana pamoja na mtoto wao.
Mwanadada huyo maarufu mtandaoni akizungumza na Wasafi TV amesema ni kweli kwa sasa wapo pamoja na hawajawahi kuachana.
"Unajua kuachana ni maneno tu tunakuwa tunaongea, halafu tukiachana sisi kwa ajili tayari ni wazazi kimaadili yetu tutakuja kukutanishwa tu na yule mtoto pale ndani, angalieni tu vitendo (tumerudiana)," amesema Gigy Money.
Utakumbuka baada ya Gigy Money kujifungua kuliibuka mvutano kati yake na Mo J ambaye ni Mtangazaji wa Choice FM kwa madai kuwa mtoto si wake baadaye zikaibuka tuhuma nyingine kuwa hatoi matunzo kwa mtoto lakini sasa wameonekana pamoja na wenye furaha.
Comments
Post a Comment