Rais Magufuli atoa angalizo Mwaka Mpya, 'Kila wanalolifanya wanasema ni maagizo kutoka juu'

Rais John Pombe Magufuli amewatakia heri ya Mwaka Mpya wa 2019 Watanzania wote na kuwaomba wadumishe umoja, amani na upendo waliouonesha katika mwaka 2018.

Akizungumza kutoka nyumbani kwake Ikulu Jijini Dar es Salaam,  Rais Magufuli amesema mwaka 2018 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa Watanzania na anatarajia kuwa mwaka 2019 utakuwa wa mafanikio zaidi kulingana na mipango ambayo nchi imejipangia kuitekeleza.

Rais Magufuli amewataka watumishi wa umma, viongozi, wakulima, wafanyabiashara, wavuvi na wafugaji kuongeza juhudi za uzalishaji mali katika mwaka 2019 huku wakipiga vita rushwa, wizi, ufisadi, ubadhilifu na kwamba anaamini kuwa uchumi wa Tanzania utazidi kupanda katika mwaka 2019.

“Ujumbe wangu kwa watumishi wa umma, ni kama nilivyotoa ujumbe kwa Watanzania wengine, wachape kazi, wajiamini, waachane na utamaduni wa kila kitu wanachokifanya kudai ni maagizo kutoka juu, huo ni ugonjwa ambao umeanza kuwapata watumishi wa umma ambapo kila wanalolifanya hata kama ni kwa mujibu wa sheria hawataki kujiamini, na wanasema hili ni maagizo kutoka juu” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameongeza kuwa anaaanza kuiona Tanzania mpya inakuja, hivyo Watanzania wakae waishi kwa sababu huu ndio wakati wa kuijenga nchi mpya.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato