Mkurugenzi wa Dodoma atoa ripoti ya utendji kazi
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Godwin Kunambi ametoa ripoti ya utendaji kazi uliofanywa na Ofisi yake katika kipindi cha mwaka 2018,
Mkurugenzi huyo ametoa ripoti hiyo wakati akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake na kusema kuwa mpango wao ifikapo mwaka 2020 na 2021 wajitegemee kwa asilimia 100 kama Majiji mengine duniani kupitia mapato ya ndani.
Pia amesema sasa hivi wameanza kulipa Maji, Umeme na Walinzi katika Shule Jijini humo, Mwaka ujao amesema wataanza kuwalipa posho zote za Watumishi Serikali kuu ibaki na mishahara tuu.
" Kwamujibu wa mpango wetu ifikapo 2020 na 2021 tujitegemee kwa asilimia 100 kama Majiji mengine duniani sisi tunataka tufikie huko, Mwaka ujao tutaanza kuwalipa posho zote za Watumishi Serikali kuu ibaki na mishahara tu" alisema Kunambi
Comments
Post a Comment