Tanzania Prisons watafuta njia kurudi kwenye ubora


Kikosi cha Tanzania Prisons msimu uliopita walimaliza wakiwa nafasi ya nne huku Kocha wao Mkuu, Mohamed Abdallah akipewa tuzo ya Kocha Bora wa msimu uliopita.

Kikosi hicho msimu huu kinawaumiza mashabiki na Viongozi kutokana na kushindwa kufurukuta kwa michezo ambayo wamecheza Ligi Kuu.

Kwa sasa Prisons wamecheza michezo 18 wameshinda mchezo mmoja pekee na kutoa sare michezo 9, wamepoteza michezo 8 na kujikusanyia pointi 12 wakiwa nafasi ya 19 kwenye msimamo wa Ligi hali iliyofanya wamtimue kazi kocha wao.

 Beki wa kikosi hicho Salum Kimenya amesema kuwa wanatambua kazi kubwa waliyonayo katika kupata matokeo hivyo wataongeza juhudi kuweza kujinasua katika nafasi waliyopo kwa sasa.

"Hatupo sehemu nzuri, tuna kazi kubwa kutoka hapa tulipo na njia ni moja tu kupata matokeo mazuri katika michezo yetu mashabiki watupe sapoti," alisema.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato