Wema Awashukuru Wanaomtakia Ndoa Njema



Staa mkubwa wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu amemshukuru Mungu kwa kuona watu ambao ni mashabiki wake wakimtakia ndoa njema.

Wema amefunguka juu ya ishu iliyosambaa mitandaoni kama moto wa kifuu juzikati kuwa ameolewa ambapo amesema amejisikia furaha mno kuona watu wakimuombea apate mume, jambo ambalo anaamini Mungu atapokea maombi yao.

Wema ameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, aliona watu ni jinsi gani walivyokuwa na shauku ya kumjua muoaji na hiyo kwake ni baraka tosha na Mungu akipenda, kitu hicho kitafanyika muda si mrefu na siyo kwa uwezo wake, bali wa Mwenyezi Mungu.


“Nimeona kwa kweli ni jinsi gani watu walivyo na upendo na mimi kwa kusema tu naolewa, hivyo naomba Mungu azipokee dua zao.

“Mimi ninachokiamini, jambo hilo litafanyika tu siku za usoni, lakini ni kwa uwezo wa aliye juu na si mwingine,” amesema Wema ambaye aliweka picha kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram zikimuonesha akiwa amechorwa ina kama bibi harusi, jambo ambalo amesema bado, lakini linakuja.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato