Ofisi ya DC Lindi yaipa kongole halmashauri ya manispaa ya Lindi

Na Ahmad Mmow, Lindi.

Kufuatia jitahada kubwa zilizofanywa na watendaji na madiwani wa halmashauri ya manispb ya Lindi. Serikali wilayani Lindi imepongeza halmashauri hiyo.

 Pongezi hizo zilitolewa juzi na katibu tawala wa wilaya(DAS) ya Lindi, Thomas Safari wakati wa kikao cha mwisho cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika juzi katika ukumbi wa mtakatifu Andrea Kagwa uliopo manispaa ya Lindi.

Safari alisema licha ya changamoto ndogondogo ambazo baadhi yake zimesababishwa na raslimali chache lakini inastahili kupongezwa.

 Alisema ushirikiano wa madiwani na watendaji wanaongozwa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Joomary Satura umesababisha mabadiliko makubwa ya maendeleo.

 Alisema ushirikiano huo licha ya kubadilisha mandhari ya manispaa, hasa kwenye miundombinu ya barabara, lakini pia umeiletea sifa na heshima manispaa hiyo.

 Alisema barabara nyingi katika mitaa ya katikati ya manispaa hiyo zimejengwa barabara za kiwango cha lami.

Hali ambayo imebadilisha haraka muonekano kuliko miaka ya nyuma. '' Kwahakika ushirikiano wenu umesababisha mambo mazuri mengi licha ya barabara lakini halma mashauri hii imewahi kuchukua ushindi wa kwanza wa mbio za Mwenge wa Uhuru.

Hakika mmeiletea heshima manispaa na wilaya ya Lindi,'' alisema Safari.

Aidha katibu tawala huyo alitoa wito kwa madiwani na watumishi wa halmashauri hiyo waendeleze mshikamano na ushirikiano huo hata baada ya madiwani hao kumaliza muda wao.

 '' Mpendane hata mkiwa nje ya uongozi, wapendeni watumishi hawa na watumishi wapendeni madiwani hawa ili hata watoto wenu wapendane,'' alisisitiza Safari.

Kwaupande wake meya wa halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Mohamed Lidume Lihumbo alitoa wito kwa watendaji waendelee kufanyakazi kwa juhudi na maarifa, huku wakiepuka kufanyakazi kwa mazoea.

 Alitoa wito kwa madiwani wenzake watoe ushirikiano kwa maslahi ya manispaa hiyo hata wakiwa nje ya uongozi walionao kwa kufichua vitendo vinavyoweza kusababisha halmashauri hiyo ikose na kupoteza mapato.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato