Lulu Diva Afunguka Kumwagiwa Maji ya Moto
Mwanamuziki wa kike wa Bongo Fleva, Lulu Abass ‘Lulu Diva’ amesema anawashangaa watu wanaosema amemwagiwa maji ya moto, kisa mume watu, jambo ambalo siyo kweli.Lulu Diva amesema kuwa, mwanaume huyo anayehusishwa naye ni kama ndugu yake.
Akizungumza Lulu Diva amesema siku zote vitu vya uongo vinavuma kuliko kitu chochote.
Amesema Baraka anayetajwa ni mtu ambaye anafanya naye kazi na amekuwa kama ndugu yake.“Hivi kama nimemwagiwa maji ya moto jamani si ningeonekana basi hata na makovu mwilini?
“Unajua siku zote kitu cha uongo kinasambaa kuliko kitu chochote maana Baraka ni kama kaka yangu kabisa, waache kupakaza uongo kama huo,” amesema Lulu Diva akipangua skendo ya kutembea na mume huyo wa mtu.
Comments
Post a Comment