Jengo la halmashauri lililotumia Sh milioni 200 ladaiwa kutekelezwa

MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme, amemtaka Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani humo kuchunguza matumizi ya Sh milioni 202  zilizotumika katika ujenzi wa nyumba ya Mkurungezi wa Manispaa ya Songea.


Agizo hilo alilitoa jana  alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye jengo hilo ambalo linadaiwa kutelekezwa kwa miaka minne bila kukaliwa na mtumishi yeyote huku fedha za Serikali zikiwa zimetumika.

 Mndeme alisema kwa taarifa alizonazo jengo hilo limejengwa tangu mwaka  2016, lakini hadi sasa halikaliwi na mtumishi yeyote jambo ambalo ni matumizi mabaya ya fedha za Serikali.

 Alisema kibaya zaidi uongozi wote wa halmashauri na wilaya upo na wanaangalia fedha za Serikali zilivyotumika katika jengo hilo bila kuchukua hatua stahiki.

 Kufuatia hali hiyo, alimwagiza Kamanda wa Takukuru kuhakikisha anachunguza kwa umakini fedha zilizotumika katika ujenzi huo, huku akimtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhamia kwenye nyumba hiyo ndani ya siku tatu.

 Kwa upande wake, Meya wa Manispaa hiyo, Abdul Mshaweji alisema nyumba hiyo imechelewa kuhamiwa na mkurugenzi kutokana na kutokukamilika kwa fensi ambayo itagharimu Sh milioni 20.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato