Trump amekatisha uhusiano wa Marekani na WHO
Bwana Trump amekosolewa nyumbani na nje ya nchi baada ya Maekani kujiondoaa kama mshirika wa Shirika la Afya Duniani - WHO.
Umoja wa Ulaya umemsihi kufikiria tena uamuzi wake huku waziri wa afya wa Ujerumani akiitaja hatua hiyo kuwa ni wenye kukatisha tamaa kwa afya kimataifa.
Mkuu wa kamati ya afya ya bunge la seneti Marekani, ambaye ni wa Republican kama Trump amesema kuwa huu sio wakati wa kujiondoa kwenye shirika hilo.
Bwana Trump amesema WHO imeshindwa kuwajibisha China juu ya mlipuko wa virusi vya corona.
The WHO, shirika linalosaidia kuimarisha masuala ya afya na kukabiliana na milipuko ya magonjwa imekuwa ikikosolewa kila wakati na Rais huyo wa Marekani kutokana na jinsi ilivyo shughulikia janga la corona.
Kumekuwa na wasiwasi mkubwa kwa wahudumu wa afya na wanasiasa, wengi wakiwa wanahofia kuwa maamuzi ya Trump yanaweza kuharibu jitihada ambazo tayari dunia imezifanya kukabiliana na mlipuko huu.
Tayari, Umoja wa Ulaya umeandika maelezo ya pamoja ikimtaka rais Ursula von der Leyen na mkuu wa masuala ya kigeni bwana Josep Borrell, ambaye alitaka Marekani kufikiria tena maamuzi yake.
Inadaiwa kuwa ili WHO ipambane na mlipuko huo vilivyo, "inahitajika kila mmoja aunge mkono jitihada inazofanya na kusaidia kadri wanavyohitaji msaada ".
"Tumeiambia Marekani kufikiria mara mbili maamuzi yake," Taarifa hiyo ilieleza aliongeza.
Waziri wa afya wa Ujerumani Jens Spahn pia alikosoa uamuzi wa Marekani na kusema kuwa anarudisha nyuma jitihada za kimataifa.
Marekani kwenyewe, amekosolewa vikali na wapinzani wake wa kisiasa kwa hatua aliyoichukua.
Seneta wa Republican Lamar Alexander alisema hakubaliani na maamuzi ya rais kwa sababu bila Marekani kufadhili katika wakati huu mgumu wa kiafya suala la upatikanaji chanjo litakuwa gumu.
"Kiukweli kuna uhitaji wa kuangalia vizuri na kubaini kama kuna makosa Shirika la Afya Duniani lilifanya kuhusiana na virusi vya corona, lakini wakati wa kufanya ukaguzi huo wa makosa ya nyuma ni baada ya kutoka katika janga hili la corona na sio katikati ya janga," alisema seneta wa kamati ya afya nchini Marekani.
Mgombea wa zamani wa nafasi ya urais na seneta wa Marekani Elizabeth Warren ameandika katika kurasa yake ya tweeter: "Maamuzi ya rais Trump kuondoka WHO wakati wa mlipuko wa dunia inaathiri jitihada za ulimwengu na kushusha hadhi ya uongozi wetu na kutishia afya za raia wa Marekani."
Anders Nordstrom, kiongozi wa zamani wa WHO alisema amesikitishwa sana na kuongezeka kwa msukumo wa kisiasa katika wakati ambao tunahitaji mshikamano wa pamoja kama dunia.
Waziri wa afya wa Afrika Kusini Zweli Mkhize anasema kuwa maamuzi hayo ni "mabaya sana".
Wanachama wa WHO wamekubaliana kuwa Mei, 19 watafanya uchunguzi huru kuhusu janga hili.
Comments
Post a Comment