Wolper avishwa pete ya uchumba na kijana huyu


Msanii wa filamu hapa nchini Jacqueline Wolper ameonekana kuvalishwa pete ya uchumba siku ya jana maeneo ya dukani kwake Sinza makaburini na mfanyabiashara wa mavazi bwana Chidy Designs.

Hilo limedhibitishwa kupitia picha na video zinazosambaa mitandaoni zikiwaonyesha wawili hao wakichumbiana, na wakati Chidy Designs akimvalisha pete hiyo alisikika akisema maneno yafuatayo  "Nakupenda, nakuhitaji wewe ndiyo furaha yangu nipo tayari kutulia kwa asilimia mia moja na nipo tayari kuwaona wanawake wote wa pembeni kama frame za baiskeli nakupenda sana"

Aidha kwa upande wa Jacqueline Wolper amesema  "Kiukweli nashindwa kuelewa hii hali imekuaje, sina cha kuongea ila nimefurahi na nimefarijika kwa kijana kama huyu kuwa tayari na kuamua kufanya hivi na naomba iwe kheri, nimempokea na nampenda sana"

Chidy Designs amesema mahusiano yao yalianza muda mrefu na Wolper ni mwanamke ambaye anamjua kwa muda mrefu.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato