Mpasuko mkubwa waibuka ndani ya kundi la kigaidi la Daesh (ISIS)


Msemaji wa Jeshi la Iraq ameeleza kuwepo mpasuko mkubwa ndani ya safu ya kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) hasa baada ya kuuawa kiongozi wa genge hilo, Abubakar Al-Baghdad.

Yahya Rasul, Msemaji wa Jeshi la Iraq aliyasema hayo jana Jumamosi ambapo akiashiria juu ya kuangamizwa Haji Taisir, mmoja wa viongozi muhimu wa kundi hilo la kigaidi, amesema kuwa licha ya kwamba kiongozi huyo wa (ISIS) alikuwa hatulii eneo moja na alikuwa hatumii simu wala mawasiliano yoyote, lakini mwishowe aliangamizwa katika operesheni kali iliyofanywa katika jimbo la Deir Ez-Zor, mashariki mwa Syria.


Sambamba na kusisitiza kwamba hivi sasa kundi la Daesh linakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kukosa kiongozi, Yahya Rasul ameongeza kwamba kuna mabaki ya wanachama wa kundi hilo ambao juhudi zaidi zinapaswa kufanyika ili kuwaangamiza kabisa. Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS), limezidisha harakati zake nchini Iraq katika miezi ya hivi karibuni ambapo makumi ya wanamuqawama wa Harakati ya Hashdu sh-Sha'abi na maafisa usalama wa serikali wameuawa shahidi na magaidi hao.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato