Waziri Jafo -"shule hii iitwe Jokate Mwegelo"



Waziri wa TAMISEMI na Mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo amekagua ujenzi wa shule ya kwanza ya kihistoria ya wasichana ambayo inajengwa kwa usimamizi wa DC wa Kisarawe Jokate Mwegelo ambaye alisimamia harambee ya ukusanyaji wa fedha za ujenzi ili kumaliza tatizo la wanafunzi wengi hasa wa kike kupata sifuri katika matokeo yao ya kidato cha nne na sita.

Fedha zilizopatikana katika harambee kupitia kampeni ya 'Tokomeza Zero' zimewezesha kukamilishwa kwa majengo 15 yakiwemo madarasa nane, nyumba ya walimu, mabweni, maabara, maktaba na vyoo”tumeweka hadi vimbweta”

Waziri Jafo ametaka shule hiyo iitwe 'Jokate Mwegelo Girls Secondary School' kwasababu ya jitihada zilizofanywa na DC huyo katika kusimamia upatikanaji wa fedha mpaka kufikia hapo ambapo Serikali itamalizia madarasa na mabweni yaliyobaki "mwezi July mwaka huu, shule ianze kuchukua kidato cha tano"



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato