DC Morogoro atoa siku 14 wenye vibanda vya nyasi kuondoka Msamvu
Mji wa Morogoro umekumbwa na taharuki usiku wa kuamkia juzi baada ya moto kuzuka katika stendi kuu ya mabasi Msamvu na kuteketeza vibanda vya wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zao katika stendi hiyo, ambapo Mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina Chonjo, ametoa agizo la siku 14 kubomolewa kwa vibanda vyote vilivyopo kituoni hapo. Mkuu wa wilaya ya Morogoro ameeleza hayo baada ya tukio la moto uliosababishwa na uunguwaji holela wa umeme katika vibanda hivyo na kusababisha kuteketeza mali zao. Zaidi ya vibanda viwili huku Mkuu wa Wilaya akimuagiza meneja wa tanesco morogoro kukata umeme unaongia katika vibanda hivyo.