Posts

Showing posts from March, 2020

Burundi imetangaza wagonjwa wawili wa kwanza wa corona

Image
Burundi imetangaza wagonjwa wawili wa kwanza wa corona baada ya Nchi hiyo kutoripoti mgonjwa tangu kuanza kwa virusi hivyo, wagonjwa wote ni Wanaume Raia wa Burundi ambao wametokea Rwanda na Dubai  “Tuna uchaguzi mkuu May 20,2020, hali ikizidi kuwa tete tunaweza kuusogeza mbele” May 20 mwaka huu, Burundi itaingia kwenye uchaguzi mkuu wa Urais ambapo Rais Nkurunziza ambaye ameitawala Nchi hiyo kwa miaka 15 sasa tangu mwaka 2005, ameahidi kutogombea tena.

Meneja wa Diamond apona Corona

Image
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Sallam SK ameweka wazi kuwa sasa ni mzima baada ya siku 14 alizokuwa ametengwa kwa ajili ya matibabu kumalizika. Sallam ambaye ni meneja wa Diamond Platnumz amesema amefanyiwa vipimo mara kadhaa ya vyote vimeonesha kuwa hana tena maambukizi ya virusi vya corona. Kupitia instagram  ameandika hivi; Nimshukuru Allah 🙏🏽 na pia niwashukuru wote mlionitumia msg, comments, DM na dua zenu. Bila kuwasahau Temeke Isolation Centre kwa kuwa bega na bega pamoja na mie bila kunichoka pale nilipokuwa nimezidiwa, na shukurani zangu zingine ziende kwa Madaktari bingwa kujua maendeleo yangu mara kwa mara na pia Serikali yangu na viongozi wake husika Wizara na Mkoa walikuwa hawana ubaguzi kutujulia hali na kutupa moyo na kutupa mahitaji tutakayo. Naomba niwape taarifa ndugu yenu, kijana wenu nimechukuliwa vipimo mara mbili na nimekutwa NEGATIVE na kwa sasa nipo huru. Ila naomba tuendelee kujikinga na kufata ushauri wa viongozi wetu na kuacha maelekezo ya ut...

Watoto 11 wa kwaya maarufu nchini Uganda wathibitishwa kuwa na corona

Image
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza visa vipya 11 vya ugonjwa wa Covid-19 nchini humo, wote wakiwa wanakwaya wa kwaya maarufu nchini humo 'Watoto Children's Choir. Kupitia matangazo ya televisheni, alisema kuwa wagonjwa wote wapya walikuwa karantini baada ya kurejea kutoa ughaibuni , ingawa hakueleza afya zao zikoje kwa sasa na walikuwa wametoka taifa gani. Mara nyingi kwaya hiyo huwa inatumbuiza katika nchi za ughaibuni kama Marekani, Canada na Uingereza. Mpaka sasa Uganda imethibitisha kuwa na wagonjwa wa Corona 44. Katika hatua za kukabiliana na maambukizi ya corona, tayari rais wa Uganda Yoweri Museveni ametagaza masharti zaidi ya kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona wiki mbili baada ya kupiga marufuku usafiri wa Umma. Katika hotuba yake kwa taifa iliyopeperushwa moja kwa moja kwenye televisheni usiku wa Jumatatu Bw. Museveni amepiga marufuku usafiri wa kutumia magari binafsi na boda boda kuanzia saa nne usiku. Mtu yeyote anayehitaji huduma za dhar...

Ulaya yaanza biashara ya mabadilishano na Iran

Image
Iran na Umoja wa Ulaya zimekamilisha mauziano ya kwanza chini ya mfumo wa ubadilishanaji bidhaa na huduma uliowekwa ili kukikiuka vikwazo vya Marekani dhidi ya Jamhuri hiyoya Kiislamu. Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani ilisema hapo jana kwamba uundwaji wa kile kinachoitwa INSTEX umefanikisha usafirishwaji wa vifaa vya matibabu kutoka Ulaya. Ikizungumza kwa niaba ya Ujerumani, Ufaransa na Uingereza, wizara hiyo imesema kwamba mfumo huo utaruhusu manunuzi mengine kuendelea. Mfumo huo ulibuniwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita baada ya Marekani kurejesha upya vikwazo vikali dhidi ya sekta ya mafuta ya Iran kufuatia hatua ya Rais Trump kujiondowa kwenye makubaliano ya kimataifa kati ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani juu ya mpango wake nyuklia. Chini ya mfumo INSTEX, bidhaa na huduma zinabadilishwa badala ya kuuzwa kwa fedha, jambo linalokwepa matumizi ya moja kwa moja ya fedha na vikwazo vya Marekani. Awali, kampuni za Ulaya hazikuwa na la kufanya zaidi ya kusitisha bi...

Mwanaume ajiandalia jeneza kisa mateso ya familia

Image
Na Paschal Malulu, Kahama Mkazi wa Ushirombo kitongoji cha Butambala Kata ya Igulwa wilayani Bukombe mkoa wa Geita Sylvester Mihayo (45) anaishi na jeneza ndani ya nyumba ambalo ameliandaa kwaajili ya mazishi yake pale atakapofariki kutokana na kile alichoeleza kuwa ni kuchoshwa na kunyanyaswa na familia yake. Aidha mwanaume huyo akizungumza na waandishi wa habari alieleza kuwa kwa takribani miaka 3  sasa, anaishi bila furaha kutokana na unyanyasaji huo ikiwa ni pamoja na kipigo kutoka kwa mke na watoto wa kuwazaa mwenyewe hali iliyompelekea kuitelekeza nyumba na kuishi kwenye karakana ya ufundi anakochomelea kwa kutumia mitungi ya gesi. Alisema kuwa chanzo cha mateso yake ni baada ya kuugua kwa muda mrefu  tangu mwaka 2018 ambapo familia ilimtenga na kumzuia kuingia kwenye nyumba yake kwa madai kuwa siyo yak wake badala yake ni nyumba ya urithi kwa watoto wake. “Ndugu zangu waandishi wa Habari mimi kujichongea jeneza siyo kwamba nitajidhuru, bali nimejitabil...

Simbachawene: Kifungo cha nje suluhisho msongamano magerezani nchini

Image
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii kabla ya kuzindua Kamati hiyo, jijini Dodoma, leo, ambayo itasimamia Utekelezaji wa Sheria ya Huduma kwa Jamii inayotoa fursa kwa wafungwa wa vifungo vidogo kutumikia adhabu hizo kwenye jamii. Pia Waziri huyo ameitaka Kamati hiyo, iweke mikakati zaidi ya kusimamia adhabu mbadala ya kifungo cha nje ili kuondoa msongamano magerezani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati meza kuu), akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii kabla uzinduzi wa Kamati hiyo, jijini Dodoma, leo.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia), akimsikiliza Katibu wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Uangalizi, Alo...

MAGAZETI YA LEO 1/4/2020

Image

Ndugu wathibitisha corona ilivyoondoa uhai wa Iddy Mbita

Image
Ibrahim Mbita amesema mdogo wake, Iddy amefariki kwa ugonjwa wa corona leo Jumanne Machi 31, 2020 katika kituo cha matibabu ya wanaougua ugonjwa huo kilichopo Hospitali ya Mloganzila, Dar es Salaam. "Familia ya Marehemu Alhaj Brigedia Generali Hashim Mbita kwa huzuni kubwa inasikitika kuarifu msiba wa mdogo wetu mpendwa IDDI HASHIM MBITA uliotokea usiku wa kuamkia leo hospitalini Mloganzila. Kutokana na tatizo lililopelekea kifo chake, CORONA, serikali itamzika mpendwa wetu leo mchana. Wawakilishi wachache sana wa familia wataruhusiwa kuhudhuria mazishi. Hakutakuwa na msiba wala matanga ya pamoja kuepuka kueneza maambukizi. Kila mtu aomboleze kwake. Dua nyingi tumuombee Iddi Allah amuweke pema peponi. Amina." Leo taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu imethibitisha kifo hicho na kubainisha kuwa alikuwa akipatiwa matibabu katika kituo hicho. "Marehemu ni Mtanzania mwanaume mwenye umri wa miaka 49 ambaye pia alikuwa akisumbuliwa na maradhi...

Halima Mdee ataka wabunge wote wapimwe corona

Image
Mbunge wa Kawe Halima Mdee amependekeza wabunge wote wapimwe CoronaVirus ili wale watakaobainika kuwa na maambukizi ya Corona wakawekwe karantini, na wale ambao hawana maambukii waendelee kufanya kazi bungeni. Amezungumza hayo alipopata nafasi ya kuuliza swali kwaajili ya ufafanuzi baada ya taarifa iliyotolewa na Spika wa bunge, Job Ndugai juu ya utaratibu mpya wa vikao vya bunge utakavyokuwa ili kukinga maambukizi ya virusi vya covid 19 kwa wabunge. “Leo wabunge wapo kwenye vyumba (utaratibu mpya wanaoingia bungeni ni 150 kati ya wabunge zaidi ya 300) kwanini tusianze na sisi tupimwe wote tukijijua tupo salama tukae hapa tu ‘debate’, hili ndio bunge la mwisho mh. kuelekea uchaguzi mkuu” Amesema Mdee. Aidha Spika Ndugai amesema kuwa wazo hilo ni zuri na litafikiriwa jinsi ya kulifanyia kazi, huku awali wakati akitoa taarifa yake amesema wabunge ambao hawatapata nafasi ya kuingia bungeni watafuatilia shughuli za bunge kupitia runinga katika kumbi na maeneo mengine yaliyopangwa. ...

Meya Iringa akabidhi ofisi na gari

Image
Aliyekuwa Meya wa Manispaa wa Iringa Alex Kimbe leo Machi 31 amekabidhi office pamoja na gari aliokuwa anatumia kwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Himid Njovu. “Baada ya kupata mukhtasari nikafikiria kwamba hata nikisema niendelee kubaki madarakani kitakachofanyika maana yake Mkurugenzi hata itisha vikao kwa hiyo nimeona ni busara kuwahurumia wananchii wa Iringa na nikabidhi ofisi ili niruhusu vikao vya halmashauri kufanyika" - Kimbe .

Hatuwezi tuka 'copy' na kupest kwa wazungu - Spika Ndugai

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amesema kuwa kama nchi haiwezi kuchukua tahadhari kama zilivyochukuliwa na Mataifa mengine duniani ya kupambana na Virusi vya Corona kwa kuwa watu wengi nchini maisha yao ni ya kubangaiza siku kwa siku. Hayo ameyabainisha leo Machi 31, 2020, Jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11 Mkutano wa 19. "Hatuwezi kuchukua measure za wazungu na kuzi copy na ku- paste hapa kwetu kama zilivyo, tutaua watu wetu, lazima tuangalie maisha yetu ya Kitanzania na kujaribu kuchukua hatua kufuatana na mazingira yetu" amesema Spika Ndugai. Aidha wakichangia hoja zao bungeni wabunge wa CHADEMA Halima Mdee na Peter Msigwa, wameishauri Serikali kuja na taarifa zote zinazohusu mwenendo wa ugonjwa wa Virusi vya Corona hapa nchini na kuangalia ni kwa namna gani kwa pamoja wataweza kukabiliana na athari ikiwemo uchumi pindi ugonjwa huo utakaposambaa zaidi.

Mpina ashtukia upimaji wa bilioni 2.6 ujenzi wa maabara ya uvuvi, atoa maagizo TAKUKURU

Image
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesimamisha malipo yote kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Petra Construction co. Limited inayojenga maabara ya kisasa ya Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) kituo cha Dar es Salaam hadi uhakiki wa gharama halisi za mradi huo utakapokamilika baada ya kubaini kuwepo matumizi mabaya ya fedha za umma kiasi cha shilingi bilioni 2.6 Hivyo Waziri Mpina ameunda tume ya kiuchunguzi itakayofanya kazi kwa siku saba na kuwahusisha wataalamu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ili kubaini ukweli wa gharama halisi za mradi huo. Akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Maabara ya  Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI)  jijini Dar es Salaam, Waziri Mpina alisema amebaini mradi unaojengwa miundombinu yake ni midogo ikilinganishwa na mkatab...

TAREMIA kuunga mkono agizo la serikali kwa kutoa msaada wa ndoo za maji tiririka

Image
Na Rebeca Duwe, Tanga MKUU wa Wilaya ya Tanga, Tobias Mwilapwa amesisitiza amri ya kuondoka wapigadebe wote katika vituo vya mabasi ikiwa ni miongoni i mwa tahadhari za kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona uliyoibuka nchini. Mkuu huyo wa Wilaya alipigilia msumari huo wakati akipokea vifaa vya kunawa mikono ndoo za maji tiririka vilivyotolewa na Chama cha wasafirishaji wa abiria wa mabasi madogo Coaster (Taremia) Mkoa wa Tanga zinazofanya safari zake Wilaya mbalimbali  Mkoani hapa. Mwilapwa alisema kuwa serikali imezuia mikusanyiko isiyokuwa ya  lazima katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya umma na kwamba amri hiyo ni pamoja na wapigadebe katika vituo vya mabasi kwa kuwa na huko ni sababu ya vyanzo vya maambukizi. “Hili nalirudia tena na   hiii ni mara ya mwisho kuwaonya wapigadebe katika vituo vya mabasi Wilayani hapa kuwa ni marufuku sitaki kuwaona.... navitaka vyombo vya usalama vitekeleze agizo hilo  kuondoa msongamano kwenye maen...

Kiongozi wa timu ya Simba Iddi Mbitta afarki dunia

Image
Aliyekuwa mjumbe wa kamati ya uchaguzi wa timu ya Simba Iddi Mbitta amefariki dunia alfajiri ya leo marchi 31 jijini Dar es Salaam.

VIDEIO: Mtanzania afariki kwa Corona Dar

Image
Mgonjwa wa virusi vya corona nchini Tanzania amefariki dunia leo Jumanne Machi 31, 2020. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Kuwasa aagiza wakala wa mbegu kuanzisha maduka ya mbegu karibu na wakulima

Image
Wakala wa Mbegu za Kilimo ASA wametakiwa kuanzisha maduka ya mbegu katika maeneo walipo wakulima ili kuwapunguzia gharama ya kuzifuta Morogoro mjini. Akizungumza na watumishi leo alipotembelea taasisi hiyo Katibu Mkuu Kilimo Bw. Gerald Kusaya amesema ASA ni Taasisi pekee ya mbegu nchini hivyo inatakiwa kuwafika wakulima wote nchini. Huduma ya mbegu bora inatakiwa na kilia mkulima hivyo ni lazima ASA wafikirie namna ya kushusha huduma zao chini kwa wakulima wadogo tofauti na ilivyo kwa sasa alibainisha Katibu Mkuu. Akitolea mfano wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro ambako ASA wanalo shamba kubwa la kuzalisha mbegu-(Msimba seed farm) Katibu Mkuu amesema wakulima wa maeneo hayo wanalazimika kwenda Morogoro mjini kununua mbegu “Naagiza muanzishe maduka ya mbegu bora katika maeneo muhimu ili wakulima wapate mbegu bora zitakazosaidia kuongeza uzalishaji wa mazao yao. Ningependa kuwepo na mahusiano mazuri kwenye Halmashauri zinazowazunguka kwa kuweka maduka ya mbegu zenu iwe nafuu kw...

Igube afanya mazungumzo kwa njia ya video na Balozi wa China nchini

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiwa Dodoma, terehe 30 Machi 2020 amefanya mazungumzo kwa njia ya video (video conference) na Balozi wa China nchini Mhe. Wang Ke.                                                         Pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya mahusiano ya pande mbili (bilateral relations), viongozi hawa walizungumzia utayari wa Serikali wa nchi zote mbili katika kupambana na mgonjwa wa COVID-19. Sambamba na utayari huo, Katibu Mkuu alimfahamisha Balozi Wang Ke kuhusu hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kupambana na kuenea  kwa ugonjwa wa virusi vya corona. Wakati huohuo, alimweleza kuhusu utayari wa Serikali kushirikiana na wadau wengine duniani ikiwemo China katika kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona. Vi...

Lipumba: Kifo cha Khalifa ni pengo kubwa CUF

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema kifo cha katibu  mkuu wa chama hicho, Khalifa Suleiman Khalifa kimeacha pengo kubwa katika chama hicho. Khalifa ambaye amewahi kuwa mbunge wa Gando kuanzia mwaka 1995  hadi 2015 amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Machi 31, 2020  katika hospitali ya Aga Khan alikokuwa akipatiwa matibabu. Profesa Lipumba ameeleza hayo leo Jumanne Machi 31, 2020 wakati akizungumza na Mwananchi.

Nay Wa Mitego: Shamsa tafadhali msamehe mwenzio amekiri makosa, embu rudi kwa mumeo

Image
Moja ya stori iliyotrend mitandaoni siku ya jana Machi 30, 2020 ni ya mfanyabiashara Chiddi Mapenzi, kumuandikia ujumbe wa kumkumbuka aliyekuwa mkewe Shamsa Ford na kujutia kumpoteza kwenye maisha yake. Sasa wakati stori hiyo inaendelea kuzungumziwa, msanii wa HipHop Nay Wa Mitego, ametumia ukurasa wake wa Instagram na kumuomba Shamsa Ford, kumsamehe mumewe na kurudiana naye. Kupitia post ambayo aliiweka na kuifuta Nay Wa Mitego ameandika kuwa,  "Cousin Shamsa Ford, wanasema samehe saba mara sabini, tafadhali msamehe mwenzio amekiri makosa, embu rudi kwa mumeo bana tafadhali, tafadhali rudi kwa mumeo" Ikumbukwe tu kipindi cha nyuma Nay Wa Mitego na Shamsa Ford, walikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi, kisha baadaye Shamsa Ford kufunga ndoa na Chiddi Mapenzi.

Wafanyabiashara wanaomiliki maduka katika stendi kubwa moshi wavunja kufuli walizofungiwa na manispaa

Image
WAFANYABIASHARA 10  wanaomiliki maduka katika eneo la stendi kubwa Moshi mkoani Kilimanjaro wamelazimika kuvunja kufuli mara baada ya kufungiwa maduka yao   na mgambo wa Manispaa kwa madai kwamba sio wapangaji halali Wakizungumzia tukio hilo kwa niaba ya wafanyabiashara hao Iren Charles ameleza kwamba wananyanyasika na Mgambo wa Manispaa ya Moshi kwa  kuwavamia na kufunga maduka yao hivyo kukazimika kuvunja kufuli hizo. Ameeleza kuwa  walifungua kesi Mahakamani ya kupinga kufungiwa maduka yao  na Mahakama kuwaruhusu kuendelea na biashara kama kawaida lakini mgambo wamekua wakifika katika maduka yao na kulazimisha kufunga kwa nguvu . Ameongeza wao  ni wamemiliki maduka hayo kwa muda mrefu wa  zaidi ya miaka 15  huku wakilipa kodi zote na kutambulika na Manispaa ya Moshi lakini sasa kilichotokea ni madalali kuingilia kukodisha maduka yao kwa garama kubwa sana. Amesema madalali ndio chanzo cha wao kukosa maduka hayo kwani zabuni ilipota...

Rais wa zamani wa Congo afariki dunia

Image
Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jacques Joaquim Yhombi Opango amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 81, Paris, Ufaransa kutokana na kuathirika na virusi vya corona, Opango aliiongoza Congo kuanzia mwaka 1977 hadi alipoondolewa kwa lazima mwaka 1979.

Breaking News: Tanzania yathibitisha kifo cha kwanza cha virusi vya Corona

Image
Wizara ya afya kupitia waziri Ummy mwalimu ametangaza kifo cha kwanza cha mgonjwa wa corona Tanzania ambaye ni Mtanzania ambaye mbali na corona alikuwa anasumbuliwa na magonjwa mengine. Endelea kutufuatilia tutakujuza zaidi

Corona yabadirishai utaratibu wa vikao vya Bunge

Image
Mkutano wa Bunge unaanza leo Jumanne Machi 31, 2020 mjini Dodoma  huku uendeshaji wa chombo hicho cha Dola ukibadilika kwa kiasi kikubwa lengo likiwa ni kuchukua tahadhari ya maambukizi ya virusi vya corona Akizungumza na waandishi wa habari Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema vikao vya mkutano huo wa 19 Bunge la 11 vitaanza kesho na kumalizika Juni 30, 2020  lakini kutakuwa na mabadiliko ikiwemo la kikao kuanza saa 8 mchana na kumalizika saa 12 jioni, badala ya kuanza saa 3 asubuhi na kumalizika saa 1:30 jioni. Amesema katika mikutano mingine walikuwa wakikutana kwa saa 9 ama zaidi lakini katika mkutano huo watakutana kwa saa zisizozidi nne. Amesema nyaraka zote kutoka serikalini  zitawafikia wabunge na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao.

Watu 3000 wamefariki kwa virusi vya corona Marekani

Image
Corona bado ni pasua kichwa duniani na sasa taarifa za vifo kwenye Nchi ya Marekani pekee ni zaidi ya Watu 3000 wamefariki huku zaidi ya 1200 wakifia New York. Idadi ya Wagonjwa kwa Marekani pekee ni zaidi ya laki moja na elfu sitini huku vifo vya corona dunia nzima vikizidi elfu thelathini na saba na Wagonjwa laki saba na elfu themanini na nne.

Tanzia: Katibu mkuu wa CUF Khalifa Suleiman Khalifa afariki dunia

Image
Katibu Mkuu wa CUF, Khalifa Suleiman Khalifa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Machi 31 2020 katika hospitali ya Aga Khan alikokuwa akipatiwa matibabu. Akizungunza na Mwananchi, mwanaye  Said Khalifa  amesema tangu Januari 2020 kwa nyakati tofauti baba yake aliugua na kulazwa katika hospitali hiyo. "Karibu mara tatu mzee alilazwa Aga Khan akipatiwa matibabu na akipata ahueni tulikuwa tunarudi nyumbani kujisikilizia. Kwa sasa siwezi kuzungumza kwa kirefu nahisi nimechanganyikiwa naomba unitafute baadaye," amesema Said. Machi 16, 2019 Khalifa akichaguliwa na baraza kuu la uongozi la CUF kuwa katibu mkuu wa pili wa chama hicho akichukua nafasi ya Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alivuliwa uanachama. Mwili wa Khalifa utazikwa leo katika makaburi ya Kisutu wilayani Ilala, Dar es Salaam.

Vijana waaswa kuunga mkono jitida za Serikali katika mapambano hidi ya corona

Image
Na Thabit Madai,Zanzibar. VIJANA Nchini wametakiwa kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya katika kukabiliana na maradhi ya mripuko ya Corona. Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar Khamis Rashid Kheir  wakati alipokuwa akigawa vifaa mbali mbali vya kujikinga na maradhi Corona huko Baraza la Vijana Mwanakwerekwe. Aliwataka vijana kuwa makini katika kupambana na maradhi hayo kwani hivi sasa yamekwisha sambaa duniani kote ‘Nyinyi ndio taifa la kesho hivyo wekeni tahadhari kujikinga na maambukizo kwa kufuata taratibu na miongozo ya serikali inayotolewa na  Wizara husika na kuacha kufanya mzaha tatizo ni kubwa,” alisema Mwenyekiti huyo. Aliwataka vijana hao kuacha kusikiliza taarifa zisizothibitiishwa na kutolewa na serikali zote mbili  kwani kufanya hivyo kutawajengea hofu. Aliwafahamisha vijana hao kutumia fursa ya kuzungumza ugonjwa wa Corona katika maeneo  yao  na kuie...