TAREMIA kuunga mkono agizo la serikali kwa kutoa msaada wa ndoo za maji tiririka



Na Rebeca Duwe, Tanga

MKUU wa Wilaya ya Tanga, Tobias Mwilapwa amesisitiza amri ya kuondoka
wapigadebe wote katika vituo vya mabasi ikiwa ni miongoni i mwa
tahadhari za kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona uliyoibuka
nchini.

Mkuu huyo wa Wilaya alipigilia msumari huo wakati akipokea vifaa vya
kunawa mikono ndoo za maji tiririka vilivyotolewa na Chama cha wasafirishaji wa abiria wa
mabasi madogo Coaster (Taremia) Mkoa wa Tanga zinazofanya safari zake
Wilaya mbalimbali  Mkoani hapa.

Mwilapwa alisema kuwa serikali imezuia mikusanyiko isiyokuwa ya
 lazima katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya umma na kwamba amri hiyo
ni pamoja na wapigadebe katika vituo vya mabasi kwa kuwa na huko ni
sababu ya vyanzo vya maambukizi.

“Hili nalirudia tena na   hiii ni mara ya mwisho kuwaonya wapigadebe
katika vituo vya mabasi Wilayani hapa kuwa ni marufuku sitaki
kuwaona.... navitaka vyombo vya usalama vitekeleze agizo hilo  kuondoa
msongamano kwenye maeneo hayo” alisema Mwilapwa.

Hata hivyo alisema pamoja na hayo tayari alishakutana na taasisi
mbalimbali za umma,binafsi ikiwemo za dini zote lengo ni kuelezana
namna ya kuchukua tahadhari kwenye maeneo yao na kutaka  elimu hiyo
kuwa ni ya kila mmoja kuifanya ajenda kwenye shughuli zake za kila
siku.

Awali mwenyekiti wa Taremia, Ismael Masud alimueleza Mkuu huyo wa
Wilaya kuwa msaada wa vyomnbo hivyo vya kunawa mikono umetolewa na
wanachama wa Chama hicho kwa lengo la kuunga mkono agizo la serikali
kumtaka kila mmoja kujiona ni mhanga wa janga la ugonjwa huo.

Kwamujibu wa Masoud ni kwamba vifaa hivyo vya maji vitawekwa kwenye
vituo vyote vinne vilivyomo katika Jiji la Tanga ambavyo ni Kituo
kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha Kange, kituo cha zamani cha
mabasi cha barabara 11 /12, Mwembe mawazo na cha Mabawa (Mabanda ya
Papa).

Aidha alieleza namna chama hicho kilivyojipanga katika kuhakikisha
wasafirishaji hao  pamoja na mambo mengine wanazingatia usalama wa
abiria wao wataweka chombo cha kunawa mikono kwa kila basi  kwa ajiri
ya anaepanda.

Kwa upande wa wapigadebe, Masoud alieleza mkakati utakaotumika kuwa ni
mabasi hayo kupakia abiria kwa zamu na kwamba la mbele litaondoka
baada ya kujaza wastani wa uwezo wake bila ya kuzidisha idadi ya watu
ili kuondoa msongamano wa kutumia wapigadebe hao.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato