Halima Mdee ataka wabunge wote wapimwe corona


Mbunge wa Kawe Halima Mdee amependekeza wabunge wote wapimwe CoronaVirus ili wale watakaobainika kuwa na maambukizi ya Corona wakawekwe karantini, na wale ambao hawana maambukii waendelee kufanya kazi bungeni.

Amezungumza hayo alipopata nafasi ya kuuliza swali kwaajili ya ufafanuzi baada ya taarifa iliyotolewa na Spika wa bunge, Job Ndugai juu ya utaratibu mpya wa vikao vya bunge utakavyokuwa ili kukinga maambukizi ya virusi vya covid 19 kwa wabunge.

“Leo wabunge wapo kwenye vyumba (utaratibu mpya wanaoingia bungeni ni 150 kati ya wabunge zaidi ya 300) kwanini tusianze na sisi tupimwe wote tukijijua tupo salama tukae hapa tu ‘debate’, hili ndio bunge la mwisho mh. kuelekea uchaguzi mkuu” Amesema Mdee.

Aidha Spika Ndugai amesema kuwa wazo hilo ni zuri na litafikiriwa jinsi ya kulifanyia kazi, huku awali wakati akitoa taarifa yake amesema wabunge ambao hawatapata nafasi ya kuingia bungeni watafuatilia shughuli za bunge kupitia runinga katika kumbi na maeneo mengine yaliyopangwa.

Sambamba na hayo Ndugai amesema tahadhari zinazoendelea kuchukuliwa katika nchi yetu kukinga maambukizi ya virusi vya Covid 19 hatizaweza kuendana moja kwa moja na zile za nchi nyingize zilizoendelea kwani watanzania wana mfumo tofauti wa maisha.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato