Ulaya yaanza biashara ya mabadilishano na Iran


Iran na Umoja wa Ulaya zimekamilisha mauziano ya kwanza chini ya mfumo wa ubadilishanaji bidhaa na huduma uliowekwa ili kukikiuka vikwazo vya Marekani dhidi ya Jamhuri hiyoya Kiislamu.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani ilisema hapo jana kwamba uundwaji wa kile kinachoitwa INSTEX umefanikisha usafirishwaji wa vifaa vya matibabu kutoka Ulaya.

Ikizungumza kwa niaba ya Ujerumani, Ufaransa na Uingereza, wizara hiyo imesema kwamba mfumo huo utaruhusu manunuzi mengine kuendelea.

Mfumo huo ulibuniwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita baada ya Marekani kurejesha upya vikwazo vikali dhidi ya sekta ya mafuta ya Iran kufuatia hatua ya Rais Trump kujiondowa kwenye makubaliano ya kimataifa kati ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani juu ya mpango wake nyuklia.

Chini ya mfumo INSTEX, bidhaa na huduma zinabadilishwa badala ya kuuzwa kwa fedha, jambo linalokwepa matumizi ya moja kwa moja ya fedha na vikwazo vya Marekani.

Awali, kampuni za Ulaya hazikuwa na la kufanya zaidi ya kusitisha biashara na Iran na kufuta miradi ya pamoja kwa hofu ya kuadhibiwa na Marekani.

Kwa mujibu wa makubaliano ya nyuklia na Marekani, China, Urusi, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, mwaka 2015 Iran iliamuwa kuiunda upya programu yake ya nyuklia ili isiweze kutengeneza bomu la atomiki.

Matokeo yake vikwazo vingi vikaondolewa na biashara na Tehran ikarejea. Lakini mwezi Mei 2018, Trump aliiondoa kwenye makubaliano hayo, na mwaka mmoja baadaye, Iran ikaanza kujivua taratibu majukumu yake kwenye mkataba huo.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato