Lipumba: Kifo cha Khalifa ni pengo kubwa CUF
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema kifo cha katibu mkuu wa chama hicho, Khalifa Suleiman Khalifa kimeacha pengo kubwa katika chama hicho.
Khalifa ambaye amewahi kuwa mbunge wa Gando kuanzia mwaka 1995 hadi 2015 amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Machi 31, 2020 katika hospitali ya Aga Khan alikokuwa akipatiwa matibabu.
Profesa Lipumba ameeleza hayo leo Jumanne Machi 31, 2020 wakati akizungumza na Mwananchi.
Comments
Post a Comment