Corona yabadirishai utaratibu wa vikao vya Bunge

Mkutano wa Bunge unaanza leo Jumanne Machi 31, 2020 mjini Dodoma  huku uendeshaji wa chombo hicho cha Dola ukibadilika kwa kiasi kikubwa lengo likiwa ni kuchukua tahadhari ya maambukizi ya virusi vya corona

Akizungumza na waandishi wa habari Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema vikao vya mkutano huo wa 19 Bunge la 11 vitaanza kesho na kumalizika Juni 30, 2020  lakini kutakuwa na mabadiliko ikiwemo la kikao kuanza saa 8 mchana na kumalizika saa 12 jioni, badala ya kuanza saa 3 asubuhi na kumalizika saa 1:30 jioni.

Amesema katika mikutano mingine walikuwa wakikutana kwa saa 9 ama zaidi lakini katika mkutano huo watakutana kwa saa zisizozidi nne.



Amesema nyaraka zote kutoka serikalini  zitawafikia wabunge na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato