Posts

Showing posts from April, 2020

VIDEO: Waziri wa katiba na sheria DKT. Augustine Mahiga afariki dunia

Image
Rais Magufuli anasikitika kutangaza kifo cha Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt.Augustine Mahiga(Mbunge) kilichotokea leo alfajiri Mei 01,2020 Dodoma, Balozi Mahiga ameugua ghafla akiwa nyumbani kwake Dodoma na amefikishwa Hospitali akiwa tayari ameshafariki. “Pamoja na umri wake mkubwa na uzoefu wa kushika madaraka katika nyadhifa mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa, Marehemu Balozi Mahiga, alikuwa mnyenyekevu na mtiifu kwa kila jukumu nililompa”-JPM TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI..USISAHAU KU SUBSCRIBE

Breaking News: Waziri Augustine Mahiga afariki dunia baada ya kuugua ghafra

Image
Rais Magufuli anasikitika kutangaza kifo cha Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt.Augustine Mahiga(Mbunge) kilichotokea leo alfajiri Mei 01,2020 Dodoma, Balozi Mahiga ameugua ghafla akiwa nyumbani kwake Dodoma na amefikishwa Hospitali akiwa tayari ameshafariki. “Pamoja na umri wake mkubwa na uzoefu wa kushika madaraka katika nyadhifa mbalimbali za Kitaifa na Kimataifa, Marehemu Balozi Mahiga, alikuwa mnyenyekevu na mtiifu kwa kila jukumu nililompa”-JPM

MAGAZETI YA LEO 1/5/2020

Image

Dawa inayoonyesha matumaini ya kutibu Corona yapatikana Marekani

Image
Dkt. Anthony Fauci ambaye anaongoza Shirika la NIAID alisema "Data inaonyesha kwamba Remdesivir ina nguvu za wazi kwamba inaweza kupunguza dalili na kusaidia mtu kupona kwa haraka" Dawa ya remdesivir inapunguza muda wa dalili kutoka siku 15 hadi siku 11 kulingana na majaribio yaliyofanywa katika Hospitali za maeneo mbalimbali Duniani. Majaribio hayo yalisimamiwa na taasisi ya Marekani kuhusu uzio na magonjwa ya maambukizi NIAID. Maelezo kamili hayajachapishwa, lakini wataalam wanasema kwamba yatakuwa matokeo bora iwapo yatathibitishwa japokuwa sio suluhu ya moja kwa moja ya ugonjwa huo.

Mgalu amtaka mkandarasi anayetekeleza miradi ya umeme vijini Morogoro, kumaliza kazi kwa wakati

Image
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amefanya ziara mkoani Morogoro na kumwagiza Mkandarasi, Kampuni ya State Grid, anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini, mkoani humo kumaliza kazi kwa wakati. Mgalu alilazimika kufanya ziara hiyo baada ya kupokea malalamiko ya kusuasua kwa Mradi husika ambapo aliwaagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kumsimamia Mkandarasi huyo ili kuhakikisha anakamilisha kazi kwa muda ulioainishwa kwenye Mkataba. Wakati wa ziara hiyo iliyofanyika Aprili 25 mwaka huu, Naibu Waziri alitembelea baadhi ya vijiji vya Wilaya za Gairo na Mvomero kujionea maendeleo ya kazi husika. Vijiji vilivyotembelewa ni Ukwamani na Nguyami (Gairo) pamoja na Komtanga (Mvomero). Kadhalika, Naibu Waziri alitembelea Yadi ya Mkandarasi iliyopo Gairo Mjini. Naibu Waziri aliwaasa viongozi na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Covid – 19 unaosababishwa na virusi vya Corona huku wakiendelea kufany...

VIDEO: Aliyeimba wimbo wa corona aibua mazito

Image
Kijana wa Jamii ya Kifugaji aitwaye Paul Siria mkazi wa Arusha ametunga Nyimbo Mbili maalum mmoja wapo ukieleza jinsi ya kujikinga na korona na wa pili kumuima Raisi Magufuli kuwaruhusu watanzania kumuabudu Mungu hata kipindi hiki cha Korona TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USISAHAU KU SUBSCRIBE

Wakili Albert Msando ashikiliwa na polisi Arusha

Image
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha Linamshikilia Wakili wa Kujitegema Albert Msando kwa Mahojiano Maalumu kufuatia Kauli yake aliyoitoa jana kuwataka waandishi wa habari kutoogopa kuripoti hali halisi ya ugonjwa wa Corona nchini Koka Moita Kaimu Kamanda Mkoa wa Arusha Amethibitisha.

Uturuki yatuma msaada wa vifaa vya matibabu Afrika Kusini

Image
Uturuki yatuma  msaada wa vifaa vya  matibabu nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kupambana  na virusi vya corona.  Katika zoezi la kupambana na maambukizi na athari za virusi vya corona, Uturuki inaendelea na  kutoa misaada ya vifaa vya matibabu  kwa mataifa tofauti ulimwenguni. Uturuki imefahamisha  kutuma msaada wa vifaa vya matibabu nchini Afrika Kusini. Wizara ya ulinzi ya Uturuki imefahamisha kuwa ndege iliokuwa na vifaa vya mamtibabu na madawa  imeanza sfari yake kutoka katika uwanja wa ndege wa Kayseri na kuelekea nchini Afrika Kusini. Imefahamishwa kuwa  vifaa hivyo ni pamoja na barakoa na vifaa vingine ambavyo huitajika katika kupambana na  virusi vya corona. Ndege hiyo ya jeshi aina ya A400M inasubiri kwa hamu kubwa nchini Afrika Kusini.

Helkopta ya NATO yapoteza mawasiliano Ugiriki

Image
Helkopta ya Canada chapa CH-148 Cyclone ambayo ilikuwa katika mpango wa ulinzi wa Umoja wa Kujihami wa NATO imetoweka katika maeneo ya bahari kati ya Ugiriki na Italia.  Katika taarifa yake jeshi la Canada limesema ilipoteza mawasiliano wakati ikiwa katika doria zake kawaida na kwamba jitihada za uokozi zinaendelea. Hata hivyo taarifa hiyo haijaeleza ilikuwa na watu wangapi, ingawa awali jeshi la Uigiriki lilisema inaaminika ilikuwa na watu sita. Taarifa za awali zinasema ilikuwa umbali wa maili 50 kutoka kisiwa cha Kefalonia cha Ugiriki.

China yaripoti visa vipya 4 vya maambukizi ya virusi vya corona

Image
Nchini China kumeripotiwa visa vipya vinne vya maambukizi ya virusi vya corona kwa Aprili 29, ikiwa ni pungufu ya vingine 22 vilivyobanika siku moja kabla.  Kwa mujibu wa mamlaka ya afya ya nchi hiyo visa vyote hivyo ni kutokoka mataifa ya nje. Idadi jumla ya maambukizi hadi wakati huu imefikia watu 82,862, pasipo na kisa kipya cha kifo. Kwa hivyo idadi jumla ya vifo nchini humo inasalia kuwa 4,633.

Trump kutoongeza muda wa jamii kujitenga

Image
Rais Donald Trump wa Marekani amesema serikali haitozidisha muda wa mwisho wa muongozo wa kujitenga baada ya kumalizika rasmi muda wake uliopangwa Alhamisi hii.  Hata hivyo watu wake wa karibu akiwemo mshauri wake, Jared Kushner, wametabiri kwamba Marekani ambayo ipo katika hali mbaya ya kimaambukizi kwa wakati huu, hali hiyo inaweza kujirudia tena Julai. Katika hatua nyingine Rais Trump amesema anampango wa kuanzisha safari za kikazi kwa kwenda Harizona wiki ijayo. Na vilevile ana matumaini ya kufanya mikutano ya hadhara ya kampeni itakayohudhuriwa na maelfu ya watu katika miezi ijayo, pamoja na kwamba wataalamu wamesema, bado kuna matumaini finyu ya uwezekano wa kupatikana kwa chanjo katika kipindi hicho. Kiongozi huyo anajaribu kuonesha sura ya matumani kwa taifa hilo katika kipindi hiki ambacho kimsingi idadi ya waliopoteza maisha kwa ugonjwa wa COVID-19 inavuka ya wale waliowawa wakati wa Vita vya Vietnam.

Vifo vya corona Marekani vyafikia Elfu 61

Image
Vifo vinavyotokana na corona vimeendelea kuongezeka USA ambapo hadi asubuhi hii wamefariki Watu 61,669,USA inaongoza kwa vifo vingi Duniani pia kwa visa ambapo leo vimefikia 1,064,572 na wamepona 147,411, Italia vifo 27,682 na visa 203,591,Hispania vifo 24,275 na visa 236,899.

Kigogo CCM amvaa Wakili Msando

Image
Diwani wa Machame Magharibi kupitia Chama cha Mapinduzi Martin Munisi, amemkosoa Wakili Albert Msando kufuatia kauli yake ya kuwataka waandishi wa habari watoke na kutoa taarifa za Corona na kwamba Arusha hali ni mbaya ili hali hata yeye hakuwa amezingatia tahadhari yoyote. Diwani Munisi ameyabainisha hayo, na kusema kuwa kauli alizozitoa Msando za kuwa Arusha hali ni mbaya zinaleta hofu kwa wananchi na kwamba kitendo cha kuwataka waandishi wawe mstari wa mbele kutoa taarifa za Corona ni makosa kwa sababu Serikali pekee ndiyo inatoa taarifa za mwenendo wa ugonjwa huo nchini. "Wakili Msando alikuwa anazungumzia suala la Corona na kugawa vifaa ili hali hata yeye hakuwa amevaa Barakoa, na kile chumba kilikuwa ni kidogo na hakukuwa na tahadhari yoyote, na aliwataka waandishi kukusanya taarifa za Corona na ni wazi kabisa watu wanakufa kwa magonjwa mengine pia" amesema Diwani Munisi. Aidha Diwani aliendelea kusema "Sasa unapowaambia waandishi waende mtaani ina maana wa...

Eto’o afunguka ushauri aliopewa na Messi

Image
Nahodh wa FC Barcelona Lionel Messi alimshukuru Samuel Eto’o kwa ushauri wake mzuri aliompatia na kumsaidia kufikia hapo kwani kuna vitu alivifanyia kazi baada ya hapo. Samuel Eto’o amefichua hayo kuwa Messi aliwahi kumshukuru kwa kumsaidia ushauri ambao uliboresha kiwango cha wakati akiwa kinda FC Barcelona lakini Eto’o hakusema alimshauri nini Messi katika mahojiano yake na DAZN. ”Siku moja alisema asante Samuel soka langu limebadilika, alitakiwa arekebishe vitu viwili au vitatu najivunia na nina furaha sana kuona hilo, ameandika historia ambayo bado haijamalizika na itakuwa ngumu kweli kuvunja zile rekodi atakazokuwa ameandika”alisema  Eto’o Eto’o na Messi walikuwa na wakati mzuri FC Barcelona kiasi cha kufanikiwa kutwaa mataji mawili ya UEFA Champions League 2006 dhidi ya Arsenal ambapo Eto’o alikuwa mchezaji bora wa mechi na 2009 dhidi ya Man United kwa ushindi wa 2-0.

Mbunge Koka awapa mizinga ya nyuki jumuiya ya wazazi Kibaha

Image
MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini, Slyvestry Koka, amekabidhi Mizinga kumi ya Nyuki Yenye Thamani ya Shilingi Milioni 1.5 kwa Umoja wa Wazazi(CCM) Kibaha Mjini kwa Ajili ya Mradi wa Ufugaji wa Nyuki. Akizungumza Wakati wa Makabidhiano Hayo, katika Ofisi za CCM Kibaha Mjini, Jana, Mbunge Koka Aliipongeza Jumuiya Hiyo kwa Kupata Mwenyekiti Mwenye Maono Makubwa ya Kuiendeleza Jumuiya Hiyo kwa Kuitafutia Miradi Mbalimbali. "Niwapongeze Jumuiya ya Wazazi Kibaha Mjini kwa Kupata Mwenyekiti Shunda Ambaye Anajitambua,Mbunifu na Mckarikaji katika Kutaka Kuacha Alama kwa Muda Aliopo Madarakani katika Utawala Wake; Aidha Mbunge Koka, Alisema kwa Hamasa ya Maendeleo ya Jumuiya ya Wazazi Imempelekea Yeye Kama Mwakilishi katika Jimbo Hilo la Kibaha Mjini Kutoa Mizinga 10 Kwa Ajili ya Kuchagiza na Kutunisha Mradi wa Ufugaji wa Nyuki Ambao Baada ya Uvunaji wa Asali Utaipatia Jumuiya Hiyo Kipato. Akizungumza Baada ya Kupokea Mizinga Hiyo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya CC...

VIDEO: Albert Msando ashikiliwa na jeshi la polisi

Image
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USISAHAU KU SUBCRIBE

VIDEO: Marehemu Jaji Agostino,wafanyakazi wamlilia

Image
Kijana wa Jamii ya Kifugaji aitwaye Paul Siria mkazi wa Arusha ametunga Nyimbo Mbili maalum mmoja wapo ukieleza jinsi ya kujikinga na korona na wa pili kumuima Raisi Magufuli kuwaruhusu watanzania kumuabudu Mungu hata kipindi hiki cha Korona TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USISAHAU KU SUBSCRIBE

RC Kilimanjaro Anna Mghwira akutwa na maambukizi ya corona

Image
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Dkt Anna Mghwira ametangaza kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo siku tatu zilizopita. "Kazi yangu inahusiana na muingiliano wa watu ndipo nikaamua  kupima na majibu yamekuja na yameonyesha kuwa ninamaambukizi ya virusi vya corona mimi mwenyewe sionyeshi dalili za ugonjwa sijisikii homa, sikohoi wala sisikii dalili yoyote ila vipimo vimekuja hivyo kwahiyo hii inaonyesha watu wengi wanatembea wakijijua kuwa wapo salama kumbe hawapo salama" alisema RC Mghwira

Ronaldo kumlipa mpenzi wake zaidi ya milioni 231 kwa mwezi kwaajili ya matumizi ya nyumbani

Image
Licha ya kua bado hawajafunga ndoa rasmi, lakini Nyota wa Soka Duniani Christiano Ronaldo, anamuhudumia mpenzi wake na mama wa mtoto wake Georginagio ipasavyo. Staa huyo amethibitisha kua anampatia mpenzi wake huyo zaidi ya shilingi Milion 273 kila mwezi ili afanyie matumizi madogo madogo ya Nyumbani. Ronaldo ameliambia Jarida la Foreign Policy , pesa izo Ni kwaajili ya matumizi binafsi ya Mwanadada huyo , kununua mahitaji yake na gharama ndogo ndogo za kila siku . "Ni Mwanamke Bora, na Mama mzuri wa wanangu, nampenda kuliko chochote" - Ronaldo ameliambia Jarida ilo

Arusha yatangaza mazishi kuhudhuriwa na watu 10

Image
Kufuatia sintofahamu inayoendelea kuhusiana na idadi ya watu wanaoruhusiwa kushiriki mazishi katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19 Duniani, Serikali ya mkoa wa Arusha imetangaza rasmi kuanzia sasa kuwa mazishi yote katika mkoa huo yatakuwa yakihudhuriwa na watu wasiozidi kumi lengo likiwa ni kupunguza msongamano wa watu katika maeneo ya makaburi.

Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhan kuzikwa jumamosi

Image
Maziko ya Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhan yanatarajiwa kufanyika Jumamosi hii Kimara King'ong'o  baada ya mwili wake kuagwa nyumbani kwake Oysterbay na kisha kwenye Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano Dar es Salaam.

Kanuni Ligi Kuu Z'bar kuboreshwa

Image
SHIRIKISHO la Soka Zanzibar (ZFF), limeanza mchakato wa kufanya maboresho ya Kanuni za Mashindano kwa ajili ya msimu ujao wa mwaka 2020/21, imeelezwa. Akizungumza na gazeti hili jana, Mkurugenzi wa Mashindano wa ZFF, Ali Mohammed Ameir, alisema katika mchakato huo wameanza na zoezi la kupokea maoni kutoka kwa wadau wa soka wa visiwani hapa ili kupatikana kwa kanuni mpya za mashindano. Ameir alisema kila mtu anayo fursa ya kutoa maoni juu ya kanuni ya kuendesha mashindano kwa msimu wa mwaka 2020/21 na ZFF inaahidi itayafanyia kazi maoni hayo ili kupata kanuni bora katika uendeshaji wa ligi zake. "Tunaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau wa soka wa hapa Zanzibar ili kupata kanuni ya kuendesha mashindano, miongoni mwa mambo katika kanuni hiyo ni muundo wa ligi utakavyokuwa, ikiwamo Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza, Ligi za Vijana, na zile za wanachama wetu ikiwamo Ligi za mikoa na wilaya," Ameir alisema. Aliongeza kutokana na changamoto ya kukutana uso kwa uso na wad...

RC Malima: Hospitali Rufani Mara mbioni, huduma kutikisa

Image
NI simulizi inayochukua miaka 40 na kadhaa, leo hii kunatekelezwa wazo la Rais wa Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere, kujengwa Hospitali ya Rufani Mkoa Mara, katika kitongoji cha Kwangwa ndani ya Manispaa ya Musoma. Mkuu wa Mkoa, Adam Malima, anasema ni uamuzi uliorejeshwa tena katika utekekezaji kupitia mikakati ya kufufua mipango mbalimbali ya Mwalimu Nyerere. Ni mradi unaoatarajiwa kunufaisha wakazi kutoka wilaya za Butiama, Rorya, Tarime, Musoma Mjini, Musoma Vijijini na Serengeti, pia majirani na wageni wao. Pia, Manispaa mjini Musoma, ambako kwenye mradi unaotekelezwa kwa jina la Mwalimu Nyerere Memorial Hospital, ulioko katika mwambao wa Ziwa Victoria. Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, anasema hospitali hiyo inajengwa katika eneo lililopo mbali wa kilomita mbili, Kusini mwa mjini Musoma, kwenye mwinuko ukipambwa na madhari ya Ziwa Victoria. Anasema, ujenzi wa hospitali hiyo ulianza mwishoni mwa mwaka jana, baada ya Rais Dk, John Magufuli, kuidhinisha zaidi ya Sh. bilion...

Wagonjwa wawili wa corona waongezeka Uganda

Image
Wizara ya Afya Uganda imesema kuna ongezeko la wagonjwa wengine wawili wa corona kati ya Watu 2002 waliopimwa jana, wagonjwa wapya ni Raia wa Uganda na Mkimbizi kutoka Burundi, hii inafanya idadi ya visa vya corona Uganda kufikia 81, waliopona ni Watu 52 na hakuna kifo.

Mario Balotelli afunguka sababu za kuikataa Juventus 2013

Image
Mshambuliaji wa zamani wa Man City Mario Balotelli ameweka wazi kuwa alikuwa mbioni kujiunga na klabu ya Juventus ya Italia akitokea Man City kabla ya kubadilisha mawazo. Balotelli aliondoka Man City 2013 baada ya kuitumikia kwa miaka mitatu na kuisaidia kushinda taji la Ligi Kuu England (EPL), amefichua kuwa Juventus ilikuwa ikimuhitaji ajiunge nao. “Adriano Galliani alinitaka nijiunge na Milan baada ya kuondoka Man City, kama unavyojua mimi ni shabiki wa Milan hivyo nilifuata moyo wangu wakati huo, Milan walikuwa nafasi ya 7 au 8 katika msimamo wa Ligi, hivyo lisingekuwa jambo zuri kwangu kwenda Juventus wakati huo” -  Balotelli Mario Balotelli ,29, ambaye kwa sasa anaichezea Brescia ya Italia, alicheza Man City kwa miaka mitatu 2010-2013 na kujiunga na AC Milan aliyodumu nayo mwaka mmoja tu kabla ya 2014 kuuzwa Liverpool ila akawa na wakati mgumu kiasi cha 2016 kumrudisha Milan kwa mkopo.

MAGAZETI YA LEO 30/4/2020

Image