Uturuki yatuma msaada wa vifaa vya matibabu Afrika Kusini
Uturuki yatuma msaada wa vifaa vya matibabu nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kupambana na virusi vya corona.
Katika zoezi la kupambana na maambukizi na athari za virusi vya corona, Uturuki inaendelea na kutoa misaada ya vifaa vya matibabu kwa mataifa tofauti ulimwenguni.
Uturuki imefahamisha kutuma msaada wa vifaa vya matibabu nchini Afrika Kusini.
Wizara ya ulinzi ya Uturuki imefahamisha kuwa ndege iliokuwa na vifaa vya mamtibabu na madawa imeanza sfari yake kutoka katika uwanja wa ndege wa Kayseri na kuelekea nchini Afrika Kusini.
Imefahamishwa kuwa vifaa hivyo ni pamoja na barakoa na vifaa vingine ambavyo huitajika katika kupambana na virusi vya corona.
Ndege hiyo ya jeshi aina ya A400M inasubiri kwa hamu kubwa nchini Afrika Kusini.
Comments
Post a Comment