Dawa inayoonyesha matumaini ya kutibu Corona yapatikana Marekani
Dkt. Anthony Fauci ambaye anaongoza Shirika la NIAID alisema "Data inaonyesha kwamba Remdesivir ina nguvu za wazi kwamba inaweza kupunguza dalili na kusaidia mtu kupona kwa haraka" Dawa ya remdesivir inapunguza muda wa dalili kutoka siku 15 hadi siku 11 kulingana na majaribio yaliyofanywa katika Hospitali za maeneo mbalimbali Duniani.
Majaribio hayo yalisimamiwa na taasisi ya Marekani kuhusu uzio na magonjwa ya maambukizi NIAID. Maelezo kamili hayajachapishwa, lakini wataalam wanasema kwamba yatakuwa matokeo bora iwapo yatathibitishwa japokuwa sio suluhu ya moja kwa moja ya ugonjwa huo.
Comments
Post a Comment