Mario Balotelli afunguka sababu za kuikataa Juventus 2013

Mshambuliaji wa zamani wa Man City Mario Balotelli ameweka wazi kuwa alikuwa mbioni kujiunga na klabu ya Juventus ya Italia akitokea Man City kabla ya kubadilisha mawazo.

Balotelli aliondoka Man City 2013 baada ya kuitumikia kwa miaka mitatu na kuisaidia kushinda taji la Ligi Kuu England (EPL), amefichua kuwa Juventus ilikuwa ikimuhitaji ajiunge nao.

“Adriano Galliani alinitaka nijiunge na Milan baada ya kuondoka Man City, kama unavyojua mimi ni shabiki wa Milan hivyo nilifuata moyo wangu wakati huo, Milan walikuwa nafasi ya 7 au 8 katika msimamo wa Ligi, hivyo lisingekuwa jambo zuri kwangu kwenda Juventus wakati huo” -  Balotelli

Mario Balotelli ,29, ambaye kwa sasa anaichezea Brescia ya Italia, alicheza Man City kwa miaka mitatu 2010-2013 na kujiunga na AC Milan aliyodumu nayo mwaka mmoja tu kabla ya 2014 kuuzwa Liverpool ila akawa na wakati mgumu kiasi cha 2016 kumrudisha Milan kwa mkopo.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato