Eto’o afunguka ushauri aliopewa na Messi


Nahodh wa FC Barcelona Lionel Messi alimshukuru Samuel Eto’o kwa ushauri wake mzuri aliompatia na kumsaidia kufikia hapo kwani kuna vitu alivifanyia kazi baada ya hapo.

Samuel Eto’o amefichua hayo kuwa Messi aliwahi kumshukuru kwa kumsaidia ushauri ambao uliboresha kiwango cha wakati akiwa kinda FC Barcelona lakini Eto’o hakusema alimshauri nini Messi katika mahojiano yake na DAZN.

”Siku moja alisema asante Samuel soka langu limebadilika, alitakiwa arekebishe vitu viwili au vitatu najivunia na nina furaha sana kuona hilo, ameandika historia ambayo bado haijamalizika na itakuwa ngumu kweli kuvunja zile rekodi atakazokuwa ameandika”alisema  Eto’o

Eto’o na Messi walikuwa na wakati mzuri FC Barcelona kiasi cha kufanikiwa kutwaa mataji mawili ya UEFA Champions League 2006 dhidi ya Arsenal ambapo Eto’o alikuwa mchezaji bora wa mechi na 2009 dhidi ya Man United kwa ushindi wa 2-0.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato