Trump kutoongeza muda wa jamii kujitenga


Rais Donald Trump wa Marekani amesema serikali haitozidisha muda wa mwisho wa muongozo wa kujitenga baada ya kumalizika rasmi muda wake uliopangwa Alhamisi hii.

 Hata hivyo watu wake wa karibu akiwemo mshauri wake, Jared Kushner, wametabiri kwamba Marekani ambayo ipo katika hali mbaya ya kimaambukizi kwa wakati huu, hali hiyo inaweza kujirudia tena Julai.

Katika hatua nyingine Rais Trump amesema anampango wa kuanzisha safari za kikazi kwa kwenda Harizona wiki ijayo.

Na vilevile ana matumaini ya kufanya mikutano ya hadhara ya kampeni itakayohudhuriwa na maelfu ya watu katika miezi ijayo, pamoja na kwamba wataalamu wamesema, bado kuna matumaini finyu ya uwezekano wa kupatikana kwa chanjo katika kipindi hicho.

Kiongozi huyo anajaribu kuonesha sura ya matumani kwa taifa hilo katika kipindi hiki ambacho kimsingi idadi ya waliopoteza maisha kwa ugonjwa wa COVID-19 inavuka ya wale waliowawa wakati wa Vita vya Vietnam.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato