Mkandarasi aagizwa kuwasaidia usafiri wafanyakazi
Na. Amiri kilagalila, Njombe
Naibu waziri wa ujenzi Elias kwandikwa ametoa maelekezo kwa mkandarasi anayejenga bara bara kwa kiwango cha lami Lot2 kutoka Moronga-Makete,kuwawezesha wafanyakazi usafiri ili waweze kufika kwa wakati katika maeneo yao ya kazi.
Waziri ametoa maelekezo hayo wakati akikagua maendeleo ya mradi mara baada ya kupata malalamiko kutoka kwa waendashaji wa mitambo katika mradi huo kutokana na kutumia gharama kubwa ili kufika sehemu ya kazi.
“Nimeelekeza hawa wakandarasi walitazame tuweke mazingira mazuri kwasababu magari yapo,waweze kuwasafirisha kwenye sehemu za kazi na mfanye kazi vizuri”alisema Kwandikwa
Hata hivyo naibu waziri huyo amewataka wafanyakazi katika maeneo hayo kutengeneza uongozi ili waweze kufikisha matatizo yao badala ya kusubiri viongozi.
“Tengenezeni uongozi wenu wenye busara sio nia ya kugombana ili kurahisisha mawasiliano na matajiri wenu kwasababu kila mmoja akizungumza itakuwa ni kelele,hii itasaidia bahati nzuri viongozi wenu ni wasikivu na watawasikilizeni kama kuna jambo mnalisema bila ugomvi”aliongeza Kwandikwa
Awali waendeshaji wa mitambo ya utengenezaji wa bara bara hiyo walisema wanahitaji kusaidiwa usafiri wowote ili kufika maeneo yao ya kazi kwani kwao imekuwa ni changamoto kubwa.
“Sisi kwakweli tutashkuru tukipata usafiri kwasababu tunatoka mbali na tunahama hama huku tukitumia nauli kubwa sisi tunahitaji hata lori sio mbaka basi,na mda mwingine hata wenzetu wasafirishaji wa abiria huwa tunawachomoa wakikwama ila sisi kwetu sisi kufika hapa bado ni shida”alisema mmoja wa waongozaji wa mashine
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Ignatio Mtawa anasema kukamilika kwa bara bara hiyo mapema kutafungua kwa kiasi kikubwa fulsa za kiuchumi.
"Tunaamini kwamba barabara hii ikikamilika basi wananchi wa Makete watanufaika sana kwasababu fulsa za kiuchumi zitafunguka na miundombinu awali ili kuwa ni kikwazo na ukizingatia tunamazao ya viazi,mbuga ya kitulo na hospital kubwa hapa kwa hiyo tutanufaika kwa kiasi kikubwa,” alisema Mtawa.
Bara bara ya Moronga-Makete yenye urefu wa km 53.5 inayojengwa kwa gaharama ya bilioni 110. 446 ikiwa ni pamoja na ongezeko la VAT inasimamiwa na Simak international kutoka Australia pamoja na kampuni ya Mac consart ingenearing and transport service ya Kitanzania kwa gharama ya mkataba wa usimamizi wa shilingi bilioni 2.68 ikiwa ni pamoja na kodi ya ongezeko la thamani huku ukitegemewa kukamilika kwa miezi 29
Comments
Post a Comment