Shabiki wa Chelsea afungiwa maisha kwa kumbagua Raheem Sterling
Klabu ya Chelsea ya England imefikia maamuzi mazito ya kutangaza kumfungia maisha kuingia uwanjani shabiki wao ambaye alionesha ubaguzi wa rangi kwa nyota wa Manchester City Raheem Sterling.
Chelsea imemfungia maisha kuingia uwanjani shabiki huyo aliyetoa maneno ya ubaguzi wa rangi kwa Sterling wakati akienda kuokota mpira wakati wa mchezo wa Ligi Kuu kati ya Chelsea na Man City December 8,2018 kwenye uwanja wa Stamford Bridge na Chelsea kupata ushindi wa 2-0.
Mashabiki wengine watano ambao walitumia lugha kali na za vitisho wamefungiwa kwa muda wa kati ya mwaka mmoja na miwili.
Pamoja na kuwa uchunguzi wa jumla kuhusiana na tuhuma hizo za ubaguzi kutokamilika kutokana na madai ya kutokuwa na ushahidi wa kutosha, lakini Chelsea binafsi ilifikia maamuzi hayo baada ya kufanya uchunguzi wao binafsi.
Comments
Post a Comment