Waziri Lukuvi atatua migogoro ya ardhi Dar


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amefanya ziara katika maeneo ya Kigogo na Msimbazi Center jijini Dar es Salaami na kurejesha kiwanja cha Bwa. Ramadhan Sudi Balega  kilicho tapeliwa na mtu ajulikanaye kama Bw. Macha  katika eneo la Kigogo.

Waziri Lukuvi amerejesha kiwanja hicho kutokana na mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka Kumi kutokana na kuwepo na utapeli katika eneo hilo huku akisisitiza kuendeleo kupambana na matapeli wa ardhi popote walipo kwani Wizara yake haitokubali wanyonge kudhurumiwa katika kipindi chake chote cha uongozi.

Lukuvi amerejesha Hati ya jengo lake na kuchukua uamuzi wa kutengua uteuzi wa msajiri wa Hati ambaye alifanya makosa ya kubadili hati kutoka kwa Ramadhan kwenda kwa Bw. Macha huku akijua kufanya hivyo ni kunyume cha utaratibu na swala hilo linatafsiriwa kuwa ni kitendo cha utapeli.

"Nataka kuwapa matumaini wananchi wote walioonewa, haki yako itachelewa tu lakini ipo siku utarudishiwa haki yako nataka kuwapa onyo watu wote ambao wanafikiri wanaweza kunyan’ganya haki ya masikini yoyote alafu Serikali isiwaone watambuwe kwamba serikali ipo macho na inashughurikia migogoro yote’’. Amesema Waziri Lukuvi.

Hata hivyo Waziri Lukuvi amewataka wananchi kutoa ushirikianao kwa kuripoti matapeli  na wadanganyifu wote waliyomo ndani ya Serikali ama nje ya Serikali ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao kama ilivyofanywa kwa msajili wa Hati aliyetenguliwa kutokana na vitendo vya kujihusisha na utapeli wa ardhi.

Kwa upande mwingine Waziri Lukuvi ametembelea eneo la msimbazi center lenye mgogoro wa muda mrefu kati ya kanisa katoliki na mmiliki wa kituo cha mafuta cha Victoria Bw. Harod Exavel ambapo eneo hilo limeonekana kuwepo na Hati mbili katika eneo moja hali hii inatokana na Kanisa kuwa na Hati iliyoipata tangu Mwaka 1965.

Hali hii inatokana watendaji wa Halmashauri ya Ilala kupitia moja ya vikao vyake  walifanya makosa na kumpa Hati Bw. Huweli ambapo Mwaka 2009, hivyo Bw. Huweli alimuuzia mmiliki wa Victoria eneo ambalo tayari Wizara  ilishalifuta hati hiyo.

Aidha Waziri Lukuvi amefafanua kuwa, kwa mujibu wa sheria ni kosa kumilikisha Hati juu ya hati nyingine au mchoro wa upimaji juu ya mchoro mwingine na kama ikitokea kufanya hivyo ni lazima Yule mwenye hati ya awali arurudishiwe kwani kuna fomu maalumu ya Serikali ( Surrender form) inajazwa na ndipo utaweza kuingia kwenye ardhi yenye hati kuipima na kuipanga matumizi.

Hata hivyo Waziri Lukuvi amewataka kukutana na pande zote mbili kati ya Kanisa Katoliki na Mmiliki wa kituo cha mafuta cha Victoria siku ya Ijumaa Septemba 2, 2019 saa tano asubuhi ofisini kwake Ilala Jijini Dar es Salaam ili kujadili namna bora ya kuweza kuutatua mgogoro huo.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato