Chile: Watu sita wafariki na wengine 40 kujeruhiwa kwenye ajali


Watu wasiopungua sita wamefariki na wengine 40 kujeruhiwa siku ya jana baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika barabara kuu ya mkoa wa kati wa Chile wa O'Higgins.

Basi liliondoka mji mkuu Santiago alfajiri Jumatatu na lilikuwa linaelekea mji wa kusini wa Temuco, umbali wa kilomita 680, lilipopata ajali hiyo.

Miongoni mwa waliofariki kulikuwa na wanawake watano na mwanaume mmoja. Uchunguzi bado unaendelea ili kubaini kilichosababisha ajali hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato