Kumbilamoto achaguliwa kuwa Meya Ilala


Diwani wa Vingunguti (CCM), Omary Kumbilamoto, amechaguliwa kuwa Meya wa Manispaa ya Ilala baada ya kumshinda mpinzani wake katika Greyson Selestin aliyepata kura 14.

Uchanguzi huo umefanyika Jumatano hii, katika kikao cha baraza la madiwani ambapo Kumbilamoto ameshinda kwa kura 41 kati ya kura 55 zilizopigwa ambapo hakuna kura iliyoharibika.

Akizungumza na waandishi baada ya uchaguzi huo, Kumbilamoto amesema anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopata na kila mmoja aliyempigia kura ambapo ameahidi kufanya kazi kwa bidii na kuomba ushirikiano ili waweze kufanikisha majukumu ya Manisapaa hiyo.

“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu  kwa nafasi hii nilioipata na kufanikisha zoezi hili la uchanguzi kufanyika na kuisha salama, nawashukuru madiwani wote mlioweza kunipigia kura za kutosha na hata msionipigia lakini mmefanikisha haki zenu za kidemokrasia.

“Kikubwa niwaombe umoja na ushirikiano katika kufanikisha majukumu ya Manispaa ya Ilala inafanya kazi na miradi yote ya mikakati ya Mh. Rais Magufuli inatekeleza kwa wakati, nitakuwa Meya wakawaida wa kutekeleza majukumu yangu kwenu ”anasema Kumbilamoto

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato