Na Omary Mngindo, Mkuranga SERIKALI imeeleza kuwa ina mpango wa kutengeneza mtambo mkubwa utaozalisha Megawati 300 za umeme, kisha kuusafirisha kutoka mkoani Mtwara kwenda Kinyerezi jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu ameyasema hayo alipozungumza na wananchi wa Kijiji cha Njopeka, Kata ya Mjawa wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, akiwa kijijini hapo mwishoni mwa wiki, ambapo alisema hatua hiyo inalenga kuboresha huduma ya umeme. Aidha alisema kuwa serikali imefanya tathmini ya fidia kwa wananchi wa maeneo ya Rufiji, Mkuranga na Dar es Salaam ambao wamepitiwa na bomba la gesi na nguzo za umeme, huku akiombaradhi kuchelewa kulipwa fidia, na kwamba zoezi hilo linataraji kuanza Julai mwaka huu. "Malipo yataanza mwezi Julai kwa wakazi waishio Mkoa wa Dar es Salaam, baada ya hapo zoezi litaendelea tena kuanzia mwezi wa nane mpaka wa kumi na mbili mwaka huu kwa wakazi wa maeneo ya Mkuranga, niwaomberadhi kwa kuchelewa fidia hizo" alisema Mgalu. Aidh...