Maelfu ya Watanzania wamuombea Rais Magufuli
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Maelfu ya Watanzania wamefanya maombi ya kumuombea Rais wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli pamoja na Viongozi wa serikali ili kuendeleza nguvu katika ujenzi wa Tanzania mpya ili kufukia uchumi wa Viwanda kama ilivyo ndoto ya Rais.
Mji wa Arusha umefurika maelfu ya watu kutoka ndani na nje ya mkoa wa Arusha pamoja na mikoa ya Kilimanjaro,Manyara,Singida,Dodoma ambao wamekusanyika kwa ajili ya kuiombea serikali na Watanzania kwa ujumla.
Mkurugenzi Msaidizi wa Redio Safina ,Hellen Lema amesema kuwa maombi hayo yanalenga kuomba Mungu azidi kumpa nguvu Rais Magufuli ili aweze kuwatumikia vyema Watanzania na taifa la Tanzania lizidi kubarikiwa na kusonga mbele kiuchumi.
Mchungaji Pascal Thomas amesema kuwa maombi hayo ya toba dhidi ya maovu mbalimbali na kuhamasisha watu kumcha Mungu na kuondokana na uovu pamoja na kuwaombea viongozi.
Kwa upande wao wananchi Ester Mremi na Joel Molel walioshiriki katika maombi hayo wameeleza umuhimu wa kuliombea taifa ili kuwa na muelekeo chanya wa kimaendeleo na kufungua milango ya kiuchumi ili waweze kufanikiwa.
Comments
Post a Comment