Mwenyekitwa Halmashauri ya Iramba mkoani Singida, Simon Tyosela ameishauri serikali kuhalalisha biashara ya akina dada wanaoujiuza, maarufu machangudoa. Amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua ukusanyaji mapato ya halmashauri mbalimbali nchini. Alitoa ushauri huo, kutokana na kauli ya Mkuu wa Mkoa, Dk Rehema Nchimbi kueleza kuwa madada poa na machangudoa wote mjini hapo kukamatwa. Dk Nchimbi alitoa kauli hiyo wakati wa Kikao Maalumu cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichopitia na kupitisha Mpango wa Bajeti kwa Mwaka 2019/2020. Tyosela amesema kutokana na halmashauri nyingi nchini kukwama kukusanya mapato, ingekuwa jambo jema kama serikali ingehalalisha biashara ya machangudoa kama zilivyo biashara nyingine. "Niseme sikubaliani kamwe na suala la ushoga. Lakini hili la machangudoa nashauri lirasimishwe ili serikali iweze kujipatia mapato,"alisema na kuongeza "Iwapo watashindwa kulipa kodi hiyo, basi watakuwa wamejiondoa kwa hiyari yao wen...
Baada ya kuishi mafichoni hususan nchini Uingereza Jamshid bin Abdullah Al Said, aliyekuwa sultani wa Zanzibar , akiwa ndio Sultan wa mwisho wa mssultani waliotawala miaka 91 kisiwani humo kutoka kwa familia ya al Busaid , alihamia katika ufalme wa Oman. Mtu huyu ambaye aliitawala Zanzibar hadi alipoondolewa katika mapinduzi ya mwezi Januari 1964 aliwasili mjini Muscat hivi karibuni. Gazeti la The Guardian linasema kwamba serikali ya Oman ilikataa maombi kadhaa yaliotolewa na Sultan huyo ili kumruhusu kuishi katika ufalme huo. Lakini ndugu yake mmoja mjini Muscat aliambia gazeti la The National mjini Abu Dhabi kwamba ombi lake la kutaka kuishi Oman limekubalika kutokana na umri wake. Amekua akitaka kuishi siku zake za mwisho katika taifa hilo la mababau zake ''na sasa anafurahia kuweza kufanya hivyo'', aliongezea. Afisa mmoja wa serikali alikataa kutoa tamko lake kulingana na gazeti la The Guardian. Uhuru na mapinduzi Jamshid bin Abdullah alizaliwa tar...
Comments
Post a Comment