RC Ayoub azitaka Mamlaka za bima kusambaza elimu kwa jamii
Na Thabit Hamidu,Zanzibar
Uongozi wa mamlaka ya Bima Tanzania umetakiwa kutoa elimu kwa jamii kukata na kutumia bima kutoka kwa watoa huduma waliosajiliwa na mamlaka husika ili kuongeza pato la taifa pamoja na kudibiti watu waoghushi huduma hiyo.
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud ametoa wito huo wakati akiungungumza na viongozi ,wadau na wananchi katika maadhimisho ya siku ya bima Zanzibar yaliyofanyika katika viwanja vya kumbukumbu kisonge mjini unguja.
Alisema endapo makampuni na wataalamu wa bima watakuwa na utamaduni wa kutoa elimu ya mara kwa mara wananchi watapata uelewa juu ya umuhimu wa huduma Bima na hawatasita kununua huduma hiyo.
"Kwa sababu mamlaka ya bima ni chombo cha ushauri kwa serikali kuhusu masuala ya soko la bima,ni matumaini yangu wananchi sasa watanunua huduma za bima,na endapo kutatokea migogoro au kutoelewana kati ya kampuni ya bima na mteja ninauhakika mamlaka yenu itakuwa tayari kulitatua na kulipatia ufumbuzi"alisema Ayoub.
Aidha Mkuu wa Mkoa amesema serikali ya Mkoa wa Mjini Magharibi inathamini jitihada za mamlaka za Bima na wadau wake katika kuendeleza maendeleo ikiwa ni pamoja na kuwasogezea wananchi huduma za bima kupitia makampuni,madalali,mawakala na wakadiria hasara wanaosajiliwa na mamlaka hiyo.
"Kulingana na ripoti ya mwenendo wa soko la bima nchini ni dhahiri kwamba juhudi za mamalaka pamoja na wadau wote wa bima zinazaa matunda kwa ongezeko la ukuwaji wa kiwango cha asilimia 7% kwa sekta ya bima inaonesha wazi kwa kushirikiana na wadau, Mamlaka inafanya kazi kwa bidii kwa lengo la kukuza soko la bima nchini'amesema Mkuu wa Mkoa.
Katika hatua nyengine Mhe Ayoub amezitaka taasisi za serikali kuwa mstari wa mbele kuvikatia bima vyombo vyao ili kuenda samabamba na mabadiliko ya sheria na maelekezo ya serikali juu ya matumizi ya bima kwa chombo mbali mbali.
Akizungumza katika maadhimisho hayo kamishna wa Mamlaka ya Bima Tanzania Ndugu Mussa Juma amesema kuwa kila mwananchi ana haki ya kupata fidia endapo atapata ajali za barabarani zitokanazo na vyombo vya moto ambapo lengo la maadhimisho hayo ni kutoa elimu ya bima kwa jamii na kuwapa miongozo ya kupata haki zao za bima pale watakapopatwa na ajali.
Alisema mamala ya Bima imekuwa na mikakati mbali mbali ili kuhakikisha inaonmgeza wateja kwa kutumia sekta za kibenki zitakazotoa huduma za upatikanaji wa bima kwa gharama nafuuu pamoja pamoja na kuzitaka kampuni zinazoingiza bidhaa chini kukata bima hapa Tanzania na si nje ya nchi kama ilivyokuwa zamani.
"Sasa hivi tumekuwa na utaratibu wa kuziagiza kampuni mbali mbali zinazoagiza bidhaa zao nje ya nchi kukata bima hapa nchini kwetu kwa mujibu wa sheria zilizopo na sio kule wanakoagiza biashara zao kama ilivyokuwa zamani" alisema ndugu Juma.
Aidha Kamishna Juma ameongeza kuwa maamlaka hiyo imekuwa na utaratibu wa kusaidia na kuchangia katika huma za kijamii ikiwemo afya ,elimu na watu wenye mahitaji maalumu kwa kutoa msaada wa mahitaji na vifaa mbali mbali kwa watu wenye mahitji maalum.
Mapema Naibu kamishna wa mamlaka ya usimamia wa Bima Tanzania Bi Khadija Issa Said amesema wamekuwa na mikakati mbali mbali ya kuhakikisha wanayafikia maeneo tofauti kutoa elimu kwa jamii na kuona wanapata uelewa wa kutosha na kuzitumia fursa zinazopatikana katika mamlaka zao.
"Nikiri zamani wananchi walikuwa na uelewa mdogo kuhusu bima kwani walijua bima ni kwa ajili ya vyombo vya moto tu kama gari lakini kutokana na mikakati yetu ya elimu tunayoitoa kwa makundi mbali mbali watu wengi wanafika katika mamlaka zetu kuleta malalamiko yao na tunawasaidia na wananpata haki zao"alisema Bi Khadija.
Katika maadhimisho hayo ya siku ya Bima Zanzibar Mkuu wa Mkoa aliongoza matembezi yaliyoanzia katika viwanja vya BAJA na kumalizia uwanja wa kumbukumbu vya muembe kisonge pamoja na kukagua shughuli za mawakala wa bima.
Comments
Post a Comment