Serikali yashirikiana na Kampuni za simu kusaidia watoto na Wanawake


Serikali imesema itaendelea kushirikiana na kampuni za simu ili kuwasaidia wananchi katika mambo mbalimbali ya kijamii yakiwemo ya Afya, Elimu  na Miundombinu.

Akizungumza  katika hafla ya uzinduzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Naibu  Waziri wa  Tamisemi,  Joseph Kandege amesema Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu ili kuwawezesha Vodacom kuwafikia watanzania wote wenye mahitaji .

 Waziri kandege Amesema Vodacom wanafanya kazi ambazo zinagusa jamii kama afya   na kuwasaidia watoto wa kike kwenda shule kwa kuwapatia vitaulo vya kujihifadhia katika hedhi, pia wameendelea kuwasaidia kina mama juu ya ugonjwa wa fistula ambayo inawapelekea wamama wengi kutengwa na jamii.

“ Serikali itahakikisha inaimarisha miundombinu ili kuhakikisha vodacom inawafikia  watu wenye uhitaji na pia tumeona jinsi walivyoweza kuwasaidia watoto wa kike na wakinamama wenye fistula juu ya kupata matibabu  ya ugonjwa huo na kugawa vitaulo kwa watoto wa kike wenye uhitaji, ambao wanakosa kwenda shuleni pindi wawapo kwenye hedhi”.

Amesema matarajio yake ni kuwa  kazi inayofanywa na vodacom  iweze kufanywa na mashirika mengine kwa kushiriki jambo kama hilo au kwa kujiunga pamoja na vodacom kufanya jambo hilo.

“ Matarajio yangu kazi hii inayofanywa na Vodacom isiwe yao na  hayo mashirika wanayoshirikiana nayo, kwani hili ni jambo la kitaifa, hivyo ni vyema mashirika mengine hata ya watu binafsi wakaendeleza juu ya hili, au wakaanzisha mambo kama haya ilikuweza kusaidia jamii zenye uhitaji kwa ujumla” .

Aidha  Mkuurugenzi wa  Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation  na Afisa Uhusiano,   Rosalynn Mwaria  amesema wamekuja kuonyesha matokeo chanya ya kazi walizokuwa wakizifanya kuanzia mwaka 2014 hadi 2017, wakiambatana na sekta binafsi pamoja serikali kwa kuwasaidia watoto na kinamama kwenye mambo mbalimbali .

Amesema hadi kufikia hapa wameshawekeza sh bilioni 11 ambazo zimewawezesha kufikia wanawake  kwa upande mkubwa  na kwa watoto wa kike kwenye sekta ya  Elimu , Afya na pia kuwawezesha kiuchumi katika mambo tofauti ili kuiendeleza Tanzania na  kuifikia jamii.

Kwa mwaka 2019 hadi 2021, Mkurugenzi huyo amesema wamejikita  katika miradi ya  watoto katika  Elimu  na pia kufanya maendeleo ambayo yatawasaidia kutunza mazingira ya Tanzania nzima.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato