RITA yazitaka bodi za wadhamini kufanya marejesho


Serikali kupitia Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA), imezitaka Bodi mbalimbali za wadhamini kufanya marejesho kwa mujibu wa sheria ya muunganisho wa wadhamini kwa muda sahihi kila mwaka.

Bodi hizo za wadhamini ni pamoja na vyama vya siasa, taasisi mbalimbali zisizo za serikali (NGOs), taasisi za kuabudu zikiwamo makanisa, vilabu vya mpira wa miguu na nyinginezo.

Hayo yamesemwa jana na Wakili wa Serikali  Mwandamizi, Edna Kamara, katika viwanja vya maonesho sabasaba ambapo amesema bodi nyingi zinafanya vizuri lakini zipo ambazo zinasuasua hivyo kuepuka sheria kuchukua mkondo wake wafanye marejesho haraka iwezekanavyo.

“Bodi ya wadhamini inatakiwa kufanya marejesho kila mwaka tarehe husika kwa kujaza fomu namba T.1.5  na kulipia ada ya Sh, 50000 kwa mujibu wa sheria ya muunganisho sura ya 318 toleo 2002 kuepuka kulipa faini.

“Hapa sabasaba huduma hizo zipo zinaendelea kwa wanaoona uvivu kufika katika ofisi za RITA wafike hapa tuwahudumie haraka,” amesema Edna.

Aidha amesema kuwa taasisi za dini zinafanya vizuri kwa kufanya mrejesho zikifuatiwa na vyama vya siasa.

“Vyama vya siasa vipo makini kufanya mirejesho yao hasa wakiongozwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), faili lao safi kabisa, lakini na vyama vingine wasipofanya hivi nafikiri watabanwa na Tume ya uchaguzi huko kwenye uchaguzi huu unaokaribia,” ameongeza Edna.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato