Ripoti mpya iliyochapishwa wiki hili kuhusu hali ya watoto duniani inaonesha kuwa kuna hatua kubwa imepigwa katika afya, elimu na usalama kwa mataifa mengi katika kipindi cha miaka 20 iliyopita. Shirika la kimataifa la Save the Children linasema hali za watoto zimeboreshwa katika nchi 173 kati ya 176, huku Singapore ikiorodheshwa kuwa kinara wa kutoa huduma bora kwa watoto. Shirika hilo lisilo la kiserikali linakadiria kuwa watoto milioni 690 wamekuwa wakinyimwa haki kutokana na kuumwa, vifo, ndoa za utotoni, mimba za mapema, utapia mlo au kutopata elimu, idadi hii ikiwa ni chini kutoka watoto 970 mwaka 2000. Nchi za Sierra Leone, Rwanda na Ethiopia zinatajwa kama nchi ambazo kwa kiwango kikubwa zimepiga hatua kuboresha maisha ya watoto katika kipindi cha miongo miwili iliyopita. Kidunia, vifo vya watoto vimepungua na kuna watoto pungufu karibu milioni 49 waliodumaa, huku China na India zikirekodi kiwango cha chini zaidi kidunia. Nchi nyingine za Afrika Mashariki ukiondoa R...