Waislam watakiwa kushirikiana kiimani katika shughuli za maendeleo
Na Rahel Nyabali,Tabora
Waislam mkoani Tabora wametakiwa kuondoa tofauti zao kwa kushirikiana katika kumcha Mwenyezi Mungu kuwa wa moja kiimani na katika shughuli za kimaendeleo ya kijamii ili kuimarisha umoja miongoni mwao bila kubaguana katika misikiti ya ibada.
Wito huo umetolewa na Sheikh wa Mkoa wa Tabora Alhaj Ibrahim Mavumbi wakati akiongea na Masheikh wa wilaya wa mkoa wa Tabora ofisini kwake amewataka masheikh kuandaa vijana wakiislamu kwa ajili ya mashindano ya kuhifadhi judhuu ambayo yatahudhuriwa na waumini wa dini mbalimbali juni 13 mwaka huu mjini Tabora.
Katika kikao hicho Sheikh Mavumbi amewaomba waumini wa dini ya kiislam kuendelea na funga yao ya mwezi mtukufu wa ramadhani kwa kufuata misingi yote ya dini bila kusahau kumcha Mwenyezi Mungu.
Aidha Wakiongea kwa niaba ya Masheikh wenzao Sheikh wa wilaya ya Nzega Mrisho Zahor na Zaimu Ramadhan kaimu Sheikh wa Urambo wameahidi kusimamia maelekezo hayo kwa kuwaelimisha waumini wao, na kuhakikisha umoja na ushirikiano katika jamii.
Comments
Post a Comment