Kauli ya Meddie Kagere baada ya kushinda tuzo mbili


Mshambuliaji wa Simba SC, Meddie Kagere amefunguka mara baada ya usiku wa jana kushinda tuzo mbili za MO Simba Awards 2019.

Tuzo hizo ambazo zilitolewa jana katika hoteli ya Hyatt Regency - The Kilimanjaro iliyopo Jijini Dar es Salaam, Kagere ndiye mchezaji pekee aliyeshinda tuzo mbili.

"Ushindi huu haujaja kwa mimi binafsi, umekuja sababu ya wachezaji wenzangu tunaelekezana jambo ambalo limenisaidia kushinda, najivunia uwepo wao” amesema.

Tuzo alizoshinda Kagere ni Mchezaji Bora wa Mwaka na Mfungaji Bora wa Mwaka.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato