Watumishi wapya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wapigwa msasa
Ofisi ya Wakili Mkuuwa Serikali kwa kushirikiana na Chuo cha Utumishi wa Umma imeendesha
mafunzo elekezi kwa watumishi wapya kwa lengo la kuwajengea uwezo na kuhakikisha inatoa huduma bora na yenye viwango.
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, yamewahusisha watumishi wapya ambao ni Mawakili, Afisa Kumbukumbu, Afisa Tehama pamoja na Afisa Habari.
Akizungumzia mafunzo hayo Mkurugenzi wa Utawala na Rasirimali Watu Bw. James Kibamba, amesema mafunzo hayo ni muhimu kwani yamelenga kuwajengea uwezo wa kimaadili watumishi wapya ili waweze kufanya kazi zao kwa mujibu wa Sheria na taratibu za Utumishi wa Umma.
“Mafunzo haya ni muhimu sana hasa kwa Watumishi wapya katika utumishi wa Umma kwa kuwa yanawasaidia kujua taratibu zote za kiutumishi ndani ya Utumishi wa Umma”. Alisema Bw. Kibamba.
Aidha Bw. Kibamba amewaasa watumishi hao kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuzingatia masuala ya kinidhamu katika nyanja zote sambasamba na kuwaheshimu watumishi wengine ili kuweza kudumisha mshikamano na ushirikiano uliopo baina ya watumishi wengine wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
Comments
Post a Comment