Bingwa wa ngumi uzito wa juu duniani Antony Joshua kuzichapa na Andy Ruiz
Bingwa wa ngumi uzito wa juu duniani,Antony Joshua amefanya mazoezi ya wazi mjini New York kuelekea pambano lake hapo kesho Juni 1 na Andy Ruiz mjini humo siku ambayo pia mabondia wa kike Delfine Persoon na Katie Taylor watapigana.
Joshua mwenye urefu wa futi sita kwa sasa anashikilia mataji matatu kati ya manne; IBF, WBA na WBO akiwa na rekodi ya kushinda mapambano yake yote 22, kati ya 21 kwa knockout.
Ruiz mwenye urefu wa futi nne amepoteza pambano moja na kushinda 32, huku 21 akishinda kwa knockout pia.
Comments
Post a Comment