MO Dewji azungumzia usajili wa Ibrahim Ajibu kwenda Simba SC
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Simba SC, Mohamed Dewji ametoa neno kuhusu mipango ya usajili ndani ya timu hiyo na kusisitiza kuwa bajeti ya usajili msimu huu itakuwa mara mbili ya ile ya msimu uliopita.
Mo Dewji amezungumza hayo muda mfupi kabla ya kutolewa kwa Tuzo za Mo (MO Simba Awards 2019) zilizofanyika jana kwenye Hotel ya Hyatt Jijini Dar es Salaam.
Amesema mipango waliyonayo kwanza ni kuhakikisha wachezaji wote wazuri wanaendelea kubaki ndani ya Simba na kisha kusajili wachezaji wengine wapya wenye uwezo.
"Wana Simba wasiwe na wasiwasi hao wachezaji wa ndani tutawabakisha kwa gharama yoyote, lakini pia tutaendelea kutafauta wachezaji wazuri na bajeti ipo," amesema.
Pia amesisitiza kuwa hadi sasa bado hawajaanza mchakato wowote wa usajili likiwemo suala la Nahodha wa Yanga SC Ibrahim Ajibu ambaye anahusishwa kujiunga na timu hiyo.
MO ameendelea kwa kusema, "Suala la Ibrahi Ajibu kwa ukweli hili jambo hatujakaa na kulimaliza, kwa hiyo kwenye wakati ujao tutajua,".
Comments
Post a Comment